Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Innocent Mungy |
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
imesema iko mbioni kuifungia mitandao ya kijamii, redio na televisheni
inayokiuka maadili ya Mtanzania.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Innocent Mungy,
alisema
kuwa mitandao hiyo ni pamoja na facebook, whatsapp na
instagram.
Alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo kutokana na kuwapo kwa watumiaji
wengi wa mitandao hiyo katika kuelekea Siku ya Mawasiliano duniani inayofanyika
Machi 15, kila mwaka.
Mungy alisema kuwa Mamlaka hiyo inafanya utafiti ili
kubaini mitandao inayoongoza kwa kulalamikiwa na wateja ili hatua zichukuliwe.
“Tangu TCRA iwezeshe kuwa na wingi wa simu na kuwezesha
kuwepo kwa mitandao mingi ya kijamii changamoto zimeongezeka, maadili
yameporomoka tofauti na miaka ya nyuma wakati kuna redio moja tu maadili
yalizingazitiwa, kwa sasa utasikia lugha za matusi kwenye radio ikiwa ni pamoja
na vipindi visivyofuata maadili na kanuni za habari, tuna mpango wakuifungia
mitandao hiyo na vyombo vya habari visivyokidhi mahitaji,” alisema.
Alisema kuwa Mamlaka hiyo lengo lake ni kuwezesha
Watanzania kwenda na wakati na kuelewa mambo mengi kwa wakati mmoja ikiwa ni
pamoja na kupata habari ndani na nje ya nchi na kuongeza ajira kwa Watanzania
kama ilivyo kwenye makampuni ya simu.
Aliwataka wamiliki wa mitandao kufuata maadili ikiwa ni
pamoja na viongozi wa dini, wazazi, kuwafundisha wananchi na waumini wao kuwa
na maadili ili kuondoa upotofu huo ambao unaweza kugeuza kizazi kisichofuata
maadili na wengine kukosa ajira kutokana na kutumia mitandao vibaya.
Aidha, alifafanua kuwa utumiaji wa simu kwa Tanzania
ulianza mwaka 1962 zikiwa ni simu zenye uzito wa kilo tatu na mwaka 1990 ndipo
zilipoingia simu za ujumbe mfupi nazo hazikuwa na matatizo ya kuporomoka kwa
maadili.
Alisema utafiti uliofanyika kwa watumiaji wa mitandao ya
kijamii unaonyesha watumiaji wanaingia bila kusoma masharti yakuingia
ambapo mitandao hiyo inatoa onyo la kutokurusha picha chafu au za mtoto chini
ya miaka mitano.
Alisema watumiaji wa simu wanafikia milioni
32,000,000 wakati vyombo vya utangazaji vimeongezeka na kufikia 123 ikiwa ni
pamoja na televiasheni 28 na redio 95. Changamoto ni kwa watumiaji kutumia
mitandao kwa njia salama ikiwa ni pamoja na kujali afya za watumiaji na kuondoa
uhalifu.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment