Monday, October 31, 2016

Please endelea kuchagua picha namba 14 ishinde!

Tafadhali ingia www.mtotomagazine.com juu kushoto palikoandikwa shindano la picha angalia picha zinazoshindaniwa halafu tuma comment ya kuchagua picha 
namba 14. 
Unatapaswa kuandika jina lako (hata moja tu sio lazima majina kamili) na email. Ni rahisi sana, asante kwa wewe ambaye umeshapiga.  Nawapenda!

Namna ya kupendezesha sebule kwa rangi ya bluu

Kwa lengo la kutengeneza sebule yenye hisia ya utulivu, muonekano wa usafi na kiwango njia mojawapo ni kwa kutumia rangi za familia ya bluu. Mara zote bluu imekuwa ni rangi freshi na inafanya ndani kuwe na uhai. Usishangae ni kwanini sebule za bluu zinaonekana nadhifu na maridadi ziadi.

Rangi mbalimbali zilizo kwenye familia ya bluu zinafanya ndani kupendeze na bila shaka kuvutie. Unaweza kutumia bluu ukutani, kwenye zulia, pazia au

Sunday, October 30, 2016

Ingia www.mtotomagazine.com upigie kura picha yangu ishinde

Hey friend!
Happy Sunday kwako.

Ninashiriki shindani la picha ya pozi bomba ya mzazi/wazazi na mtoto/watoto na nina furaha kubwa kuwa picha yangu na watoto imepita mchujo wa awali, ambapo imepewa namba 14.

Nakuomba tembelea www.mtotomagazine.com halafu bofya pale juu kushoto palipoandikwa shindano la picha. Halafu tuma comment uandike PICHA NAMBA 14 ili ishinde.





Asante barikiwa sana msomaji wangu!

Thursday, October 27, 2016

Zingatia mambo haya matatu unaponunua kioo cha kupendezesha


Huenda  uko kwenye mchakato wa kupendezesha nyumba mpya au unaboresha ya zamani, kioo ni pambo muhimu unalohitaji angalau kwenye kila chumba. Ukisema kioo tu inaonekana kama ni kitu rahisi, madukani vipo vingi vidogo, vikubwa na vya maumbo mbalimbali. Hata hivyo ikifika wakati unapotaka kununua, kupata kilicho sahihi kwa chumba fulani pasipo changamoto, zingatia mambo haya matatu.

1. Urefu wa ukuta – Kabla ya

Tuesday, October 25, 2016

Fimbo nzuri za kutundikia pazia zina vigezo hivi

Kwa takriban miaka 10 iliyopita matumizi ya fimbo au wengine wanaita bomba imekuwa ni njia ya kawaida zaidi ya kutundikia pazia. Zinafanya utundikaji uwe rahisi na uvutie.

Unapotaka kununua fimbo nzuri za pazia zingatia vigezo hivi.

Malighafi
Zipo fimbo zilizotengenezwa kwa plastiki, chuma, aluminiam na miti.
Kwa uimara na kudumu muda mrefu, fimbo nzuri za pazia zinatakiwa zile za

Saturday, October 22, 2016

Uzuri wa zulia lenye michoro kama ya kwenye ngozi ya wanyama

Kupendezesha nyumba kwa vitu vyenye rangi kama za michoro iliyopo kwenye ngozi za wanyama hakujawahi kupitwa na wakati. Kama unapenda mazulia lakini hujui namna ya kupamba kwa kutumia yale yenye michoro kama ya kwenye ngozi za wanyama, kwenye makala hii utazijua mbinu zote.

Mazulia haya kwa muonekano wake tu yana uzuri wa

Wednesday, October 19, 2016

Namna ya kupendezesha nyumba ionekane ya gharama ila kwa bajeti ndogo

Wengi tunapenda ndani ya nyumba tunamoishi kuwe kuna mvuto. Ila bado tunajiuliza kama itawezekana kwa bajeti iliyopo ambayo bila shaka ni ndogo. Wala isikupe shaka! Katika makala hii nitakuonyesha njia tano ambazo zitapafanya nyumbni kwako paonekane kwa gharama bila bajeti ya

Monday, October 17, 2016

Namna ya kusafisha milango ya ndani ya mbao

Milango katika nyumba nyingi mara nyingi haifikiriwi kufanyiwa usafi. Ni ile ya vyumba vya kulala, ya makabati ya nguo, ya mabafu, wa jikoni na wa stoo. Labda ni kwasababu haipati uchafu kwa wingi na kwa muda mfupi kama maeneo mengine ya ndani. Hata hivyo inapaswa kusafishwa kila baada ya kipindi fulani. Ikiwa ni pamoja na eneo lenye kitasa linapaswa kusafishwa na

Wednesday, October 12, 2016

Dondoo za kupendezesha pembeni mwa luninga

Kupendezesha pembeni mwa luninga inaweza kuwa changamoto na pia baadhi wanadhani kwamba wakishaiweka iwe ni ukutani au juu ya kabati basi inatosha. Bahati mzuri ni kwamba ujio wa luninga za vioo flati na nyembamba yaani zisizo na kichogo kama zile za zamani, unafanya kazi ya kupendezesha pembeni mwake iwe rahisi.
Hapa hebu tuangalie dondoo tano za

Tuesday, October 11, 2016

Namna ya kuleta ushirika wa rangi za pazia na za viti/sofa

 
Aidha unapamba upya au ni bahati kwamba ndio umekamisha ujenzi wa nyumba yako, bila shaka ni wakati wa kufikiria rangi za vitu ambavyo utahitaji kwenye kila chumba. Vyumba vikubwa kama vile sebule na chumba cha kulala cha wakuu wa familia ni

Tuesday, October 4, 2016

Njia kuu 4 za kuaminika ili kuongeza nafasi kwenye chumba cha kulala

Inawezekana umepanga nyumba yenye chumba kidogo cha kulala. Na kama tujuavyo nyumba nyingi za kupanga hazina ile mifumo ya kukuwezesha kupangilia vitu vyako kama vile makabati ya nguo na kadhalika. Hata hivyo unaweza kuishi vizuri mno kwenye chumba hicho kidogo endapo utafahamu jinsi ya kukiweka katika muonekano sahihi.

Kuna mbinu nyingi ya kukipanga chumba cha

Monday, October 3, 2016

Grauti za rangi zinavyopendezesha eneo lenye marumaru




Sio siri kuwa marumaru imekuwa ni malighafi ambayo inapendwa na wengi kwenye sakafu na kuta kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuhimili uchafu na unyevu. Kile kinachounganisha marumaru moja na nyingine kinahusika sana kwenye muonekano na usafi wa sakafu au ukuta wa marumaru.

Mhandisi David Sembuyagi wa kampuni ya Ujenzi Bulk Build simu 0715 630 073 anatuelezea jnsi malighafi ya