Thursday, May 6, 2021

NAMNA YA KUEPUKA WIVU

 FOLLOW Instagram @vivinavisa vyake


Ili uweze kuwa na mahusiano mazuri ni lazima ujifunze namna ya kuepuka wivu. 

Kila mtu ameumbwa na wivu tofauti kati ya muonekano wa wivu wa mmoja na mwingine ni ninsi unayemdani hana wivu anavyoweza kuukabili wivu wake na yule unayemuona ana wivu ni jinsi asivyweza kuukabili wivu wake.

Hivyo basi ili kuepuka kuonyesha kiwango cha wivu wajo waziwazi ili hatimaye uwe na furaha na pia na mahusiano mazuri na watu inabidi ufanye yafuatayo:
1. Usijilinganishe na safari ya mwingine maana kila mtu bhapa duniani ana safari yake ya kipekee.
2. Huenda hauko kwenye hatua kama ya unaowaonea wivu kwa ajili |Mungu amekupangia kuna jema lako linakusubiri
3. Muonekano wa wengine unaweza kuona ni mrahisi kumbe hujui stori yao yote.
4. Epuka kufuatilia ya wenzingine maana kunaweza kukuvuruga kazana na kufanya yako.
5. Chagua kuangali na kufanyanya yake yakupayo furaha.

Kama unatatizo linalopelekea kukosa furaha na maendeleo ya nafsi yako njoo tuzungumze simu 0755200023


Tuesday, May 4, 2021

MSHAURI AKIKUPA MAJIBU HAYA NI KWAMBA HANA MSAADA UNAOHITAJI

 FOLLOW INSTAGRAM @vivinavisavyake



Wengi wetu tumeshapitia changamoto za kimahusiano ambapo kumueleza mtu tunayemuamini huwa inatupa ahueni au msaada ambao utatuvusha.

Kama huyo unayemuamini na kumwendea kumueleza anakupa majibu haya ina maanisha kwamba aidha jambo lako ni kubwa sana kwake kuweza kulichakata na kukushauri cha kufanya ama hataki kujishuhulisha nalo.

Hivyo anaweza kukupa baadhi au mojawapo ya sentensi hizi. 
1. Kila kitu kinatokea kwasababu.
2. Liombee tu
3. Muda utasema
4. Achana nalo
5. Usiliongelee tena
6. Utakua sawa ukijaribu kulisahau
7. Acha kulifikiria utajisikia vizuri
8. Kuwa imara tu
9. Maisha ndivyo yalivyo
10. Ambacho hakijakuua kinakufanya imara
11. Ingeweza kuwa mbaya zaidi.

Ukishaona majibu hayo hapo juu, aga tu kwa uzuri na usirejee kwake kwani hutapata msaada unaotaka.
Muhimu ni kwakuwa umeshajua basi usikate tamaa bali tafuta msaada kwingine.

Kama una changamoto ya mahusiano njoo tuzungumze simu 0755200023