Jinsi ya mwanamke kuonekana bomba na gauni
jekundu
Nyimbo zimeimbwa, sinema
zimechezwa na maonyesho ya mavazi yamefanyika yote ni juu ya gauni jekundu.
Gauni jekundu moja kwa moja linakufanya uchomoze nje ya jopo kwa hivyo kujiamini
ni kitu kinachotakiwa wakati umelivaa. Nyekundu
ni rangi ya mahaba. Mfikirie mdada ndani ya nguo nyekundu ambaye anafanya
shingo ya kila mwanaume mwenye damu nyekundu imgeukie.
Nyekundu ni rangi moja ambayo wanawake wachache wanathubutu kuvaa. Nyekundu ni rangi inayoambatana na mapenzi, na mategemeo ya uhai.
Mwanamke anayevaa nyekundu sahihi anaonekana bomba kwa kila amtazamaye. Nyekundu hiyo ni ile inayoendana na umbo lake na rangi ya ngozi pia.
Angalia, kuna nyekundu za kuwaka na zilizopoa.

Baadhi ya
vitu vya kuzingatia kabla ya kuthubutu kuvaa gauni lako jekundu la mahaba, ambalo
unatamani mara kwa mara kulivaa ni hivi:
- Angalia ni muda gani wa siku unapovaa rangi nyekundu. Wakati wa mchana chagua nyekundu kama rangi kuu lakini kuwe na rangi nyingine ndogo. Kama unavaa gauni jekundu usiku vaa nyekundu tupu kwa ajili inaonyesha mahaba zaidi.
- Nyekundu zilizopoa zinapendeza kwa ngozi mng’avu, chagua nyekundu kuendana na rangi ya ngozi yako. Vaa nyekundu za kuwaka kama rangi ya ngozi yako ni nyeusi.
- Kama wewe ni mwanamke mwenye mwili mdogo vaa nyekundu za kuwaka na za kushika mwili. Hii itakufanya uonekane kwa ajili mwili wako ni mdogo. Unaweza pia kuvaa zenye michoro ili kuleta mvuto kwa mtazamaji. Chagua nyekundu yenye michoro kwenye kiuno au vaa mkanda wa rangi za pundamilia au chuichui ili kuelekeza macho ya mtazamaji kwenye nyonga.
- Kwa wanawake wenye maumbo makubwa, vaa nyekundu zilizopoa kama ya damu ya mzee au nyekundu ya mvinyo mwekundu ili kuondoa macho ya mtazamaji kwenye mwili wako. Pia waweza chagua nyekundu yenye michoro kuanzia kwenye makalio shuka chini ili kufanya macho ya mtazamaji yasielekee kwenye tumbo lako kubwa.
Jijue.
Unapendeza
kwenye nyeusi au bluu ya kuelekea weusi au kijivu? Kama ndio basi utapendeza
kwenye nyekundu zilizopoa. Kata tikitimaji na uangalie ile nyekundu iliyopo
ndani yake. Hii nyekundu ya tikitimaji ni ile iliyopoa ambayo itakupendeza
wewe. Chagua nyekundu za aina hii.
Kama
unapendeza kwenye rangi ya chugwa kuliko kwenye nyeusi ina maana utaonekana
bomba kwenye nyekundu ya kuwaka. Angalia nyanya iliyoiva. Hii ni nyekudu ambayo
itakufaa sana wewe.
Mara unapojua nyekundu yako basi anza kujijengea kabati la nguo la nyekundu.
Sasa tayari una nyekundu zako, chagua rangi nyingine chache ambazo zitaendana na nyekundu na rangi yako ya ngozi. Zangi za wanyama kama chuichui na pundamilia zinaendana vyema na nyekundu.

Vitupio
vya kuvaan na gauni jekundu
Gauni jekundu halihitaji vitupio kwa
sana kwa ajili tayari nyekundu ina mvuto. Uwe makini unapotupia na gauni
jekundu kwani ukiremba sana utakuwa kama mdoli. Vaa gauni jekundu na urembo wa
dhahabu au silva. Usivae vyote kwa pamoja. Unaweza kutupia kimkufu na bangili
pia paka rangi ya kucha na mdomo inayoendana na nyekundu ya nguo yako. Tena
kama ukitupia na mkanda mweusi itakuwa bomba zaidi.
Zaidi ya viatu vyeusi gauni jekundu
waweza pia kuvaa na viatu vya rangi ya silva.
Nyekundu
imejaaliwa, ni rangi inayoleta mvuto. Si rangi ya mtu anayetaka kujificha kwenye
jopo. Lakini kama unataka kuwa nyota, kama umechoka kufuata mkumbo, kama unatk
kuwa tofauti basi nyekundu ni rangi ya kuvaa.
Makala hii imeandaliwa na Vivi O.Machange 0755 200023
Makala hii imeandaliwa na Vivi O.Machange 0755 200023
No comments:
Post a Comment