Sunday, January 3, 2016

KUTOKA KWA MDAU: Sikuwa na Jiko la Ndani Nikapunguza Sebule Kutengeneza Open Kitchen

Ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa amempa kila mmoja uwezo wa kubuni kwa kiasi chake. Mdau wangu huyu hakuwa na jiko la ndani. Alichoamua kufanya ni kupunguza ukubwa wa sebule na hatimaye yuko kwenye mchakato wa kumalizia open kitchen yake. Tazama picha
Mfano wa open kitchen
Open Kitchen ni jina ambalo linatumika kwa jiko ambalo halina kizuizi cha ukuta kati ya jikoni na sebuleni au dining.

Uzunguni walibuni hii kitu kwani mpishi alitaka ashiriki yanayoendelea sebuleni..kwenye open kitchen ni kama there is nothing to hide wakati unapopika.
Hii hapa open kitchen ya mdau wangu inayoendelea kutengenezwa. 

Kiukweli ukiwa na kabati la vyombo dining huhitaji kuwa na makabati mengi jikoni. Kwahivyo huyu mdau akiongezea kabati chache za juu zinatosha kuhifadhia vile vyombo vya kuandaa na kupikia chakula. Vingine vyote kama vile sahani, glass, majagi na kadhalika vinaenda kwenye kabati la vyombo lililopo dining (hii nime assume sio yeye kaniambia)


 Asante sana mdau wangu naamini wapo watakaofaidika na ubunifu wako. Open kitchen yako itakapokamilika usisahau kunitumia tena picha. 

Nawe msomaji wangu usiwe mchoyo naamini una jinsi utakavyoweza kutuelimisha kuhusu decor mbalimbali za mahali unapoishi iwe ni nyumba au bustani, hata kwa decor ndogo kama vesi ya maua we usijali nitumie tu picha. Kwa mawasiliano piga/whatsapp 0755200023. Asante sana

2 comments:

  1. Napenda sana open kitchen. Hivi Dada Vivi natakakujua kuweka store jikon na kuweka makabati makubwa ipi ni nzuri?

    ReplyDelete
  2. Hey Matola...Stoo ya jikoni ni muhimu sana kwa kuhifadhia vyakula vingi na kuliweka jiko kwenye mpangilio ili kuepusha mrundikano. Pia stoo hiyo unaweza kuweka vyakuwa kama vitunguu vikiwa wazi ili visiharibike mapema ambapo kwenye makabati huwezi. Kama una dining ya kutosha kuweka kabati la vyombo, ukiwa na makabati machache tu jikoni inatosha.

    ReplyDelete