Kanye West ametekeleza matakwa ya kesi iliyokuwa
ikimkabilia ya kumpiga paparazi.
Paparazi huyo alimtaka West kukutana naye palepale
alipompiga na
kumuomba msamaha na kisha salamu.
Sasa picha zimeibuka zikionesha mwanamuziki huyo wa
mdundo wa kufoka akitabasamu na paparazi aliyemshtaki.
Mpiga picha wa magazeti ya umbea Daniel Ramos alimshtaki
West kwa kumshambulia baada ya kumuuliza kwanini alikuwa anasusia maswali ya
waandishi wa habari nje ya uwanja wa Los Angeles..
Wakili wake ,Gloria Allred amesema kuwa wawili hao
walikutana na West akaomba msamaha.
Kanye West ametekeleza matakwa ya kesi iliyokuwa
ikimkabilia ya kumpiga paparazi.
Hata hivyo vipengee mahsusi ya makubaliano hayo na
msamaha hayajabainika.
Kwa upande wake wakili anayemwakilisha bwana West ,Shawn
Holley, amenyamaza kimya!
West, 37, aliomba mahakama imuonee huruma kwa kosa hilo
la kumvamia mtu.
West anachunguzwa.
BBC
No comments:
Post a Comment