Friday, April 21, 2017

Namna ya kuchagua mtindo wa wallpaper

 
Tunaweza kusema kuwa wallpaper ndio habari ya mjini kwa sasa kwa ajili ya kupendezesha vyumbani kwenye nyumba nyingi za kisasa hasa  sebule. Tatizo lililopo ni changamoto ya mtindo upi ndio sahih kutokana na uwepo wa wallpaper za rangi na michoro mingi mno. Hadi zile flati yaani zisizo na mchoro wowote.

Elimika na dondoo hizi za namna mnunuzi anayetaka kupamba kwa
pambo hili anavyoweza kununua ya mtindo sahihi kwa chumba sahihi.

Unapotaka kupamba kwa wallpaper kuna maswali kadhaa ya mitindo ya  wallpaper unatakiwa uweze kujijibu. Je chaguo zuri kwako ni wallpaper yenye michoro au iliyo flati? Jibu hapa linategemea na ladha binafsi ya mwenye kutaka kupamba. Wallpaper yenye michoro hata kama ni ya rangi sawa na ya wallpaper yenyewe, kwa kawaida inasaidia kuficha makosa yoyote yaliyopo ukutani.

Wallpaper flati inakupa wigo mpana wa muonekano wa kung’aa na metaliki. Lakini kwa ujumla mimi Vivi kama muuzaji na mpambaji nimeona wateja wangu wengi zaidi wakipendelea wallpaper zenye michoro kuliko zile za flati.

Zingatia kiasi cha mwanga kwenye chumba husika kwa wallpaper ya rangi nzito au nyepesi  ili kiwango kisiathirike iwe ni asubuhi, mchana au usiku.

Je ni ukuta wa chumba gani unaotaka kuubandika wallpaper?
-Kama ni chumba cha kulala cha wanandoa, wallpapaer  zenye maua ndiyo zinafaa zaidi kwani zinaleta hisia ya mahaba.
-Kama ni sebule yenye mapambo ya mtindo wa kisasa, wallpaper zenye michoro ya rangi nzito, metaliki, ya kung’aa na ya mguso wa mtelezo  ndio zinafaa zaidi kwani ndizo zinazoonekana  ni za kifahari.

Swali lingine la kujiuliza ni kwa staili unayotaka kubandika hiyo wallpaper. Staili zote hazileti muonekano unaofanana, sawa eeh? Kwa mfano kubandika wallpaper kwenye ukuta mmoja tu kati ya nne za chumba sio sawa na kubandika kwenye kuta zote pengine na dari. Chagua wallpaper yenye rangi nzito kama unabandika kwenye ukuta mmoja tu mfano ule wa luninga au wa tendego. Staili ya wallpaper yenye rangi za namna hiyo, metaliki na mtelezo itatoa muonekano wa kiwango na kuvutia. Vilevile wallpaper za mtindo huu zinapendeza pia kwenye dari.
Chumba kidogo kinapendeza wallpaper isiyo na michoro au maua laa kama inayo basi yawe ni yale madogodogo. Wakati kikubwa kikipendeza kwa wallpaper yenye michoro na maua makubwa. Na vilevile kwenye kabati la maonyesho au vyombo likipendeza kwa wallpaper za rangi za mwanga na moja.
Kwahivyo ukishakuwa na vigezo hivi kichwani, ni rahisi kuchagua wallpaper sahihi.Tuna mitindo zaidi ya 100 ya wallpaper. 

Mawasiliano 0755 200023 tupo Sinza Kijiweni

No comments:

Post a Comment