Wednesday, October 14, 2015

Mapambo tofauti na maua ambayo unaweza kuweka katikati ya meza

Picha hizi ni kwa ajili ya kukupa mawazo tofauti ya mapambo unayoweza kupambia katikati ya meza yako mbali na maua. Karibu twende pamoja...
Bakuli la mtunda yasiyokuwa halisi

Bakuli mkubwa tupu 
Kisanamu kama hiki cha mnyama twiga. Kwa picha zaidi zama

Tuesday, October 13, 2015

ASKARI AUAWA KWA KUCHOMWA KISU NA MTANGAZAJI WAKIMGOMBEA MSICHANA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI BAA

Askari polisi wa mjini Babati, Mkoa wa Manyara ameuawa kwa kuchomwa kisu na mtangazaji mmoja wa redio kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Picha mbalimbali za mageti yaliyopo kwenye chati kwa sasa

Geti linapokuwa zuri pasipo chembe ya shaka hata thamani ya nyumba inaongezeka
Ukiwekea paa juu ya geti lako kuna faida 3 za haraka. Moja ni kuongeza mvuto, pili ni kumwekea kivuli mgeni wa miguu anaposubiri kufunguliwa iwe kuna jua kali au mvua na tatu ni kuwezesha geti lidumu muda mrefu kwa kulizuia na maji ya moja kwa moja ya mvua ambayo baada ya muda yanasababisha kutu.

 Hili geti lina rangi za kutulia, haling'ai sana na wala sio giza

 Rangi ya njano na nyeusi imelifanya geti livutie na kung'aa
Kwa asiyependa mng'aro kwa sana anaiua kidogo ile njano

Monday, October 12, 2015

Sofa za kisasa sokoni kwa sasa ni za shape ya L



Kama kawaida yangu ya kupita sehemu mbalimbali ili kukuletea vitu vizuri kwa ajili ya nyumba yako leo nakuletea sofa za kisasa zilizopo sokoni. Sofa hizi ni zile zenye umbo la L. Sofa hizi zimependwa zaidi kwa sababu kadhaa:

Saturday, October 10, 2015

Kali ya kampeni......Dovutwa kuunganisha elimu ya msingi na sekondari hadi darasa la 10, baada ya hapo ni chuo kikuu

CHAMA cha United People's Democratic Party (UPDP), juzi kimezindua kampeni za mgombea urais wa chama hicho, Fahmi Dovutwa, uliofanyika katika Viwanja vya Garden, Kilwa Kivinje, Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi.

Dovutwa alisema
"Katika sekta ya elimu nitaweka

Mwanamke mfanyakazi wa ndani toka India akatwa mkono Saudia.......Ni kwasababu alikuwa anajaribu kutoroka

Ajira shida, ujobless nao shida, lipi jema sasa....Wizara ya mashauri ya kigeni ya India imelalamikia serikali ya Saudi Arabia baada ya mwanamke raia wa India kudaiwa kukatwa mkono na mwajiri wake mjini Riyadh.

Mkono wa Kasturi Munirathinam mwenye umri wa miaka 58 alikatwa mkono wa kulia na mwajiri wake alipojaribu kutoroka.

Tuesday, October 6, 2015

Baraza la Maaskofu TEC laidhinisha ibada ifanyike jumamosi tar 24 ili kuruhusu waumini wakapige kura jumapili......Askofu asema kumuita mwenzako oil chafu ni kumdharau muumba


Askofu Severin Niwemugizi

BAADHI ya Majimbo ya Kanisa Katoliki nchini, yametoa ruhusa maalum kwa mapadri yakiwataka kuendesha ibada zao siku ya Jumamosi ya Oktoba 24 badala ya Jumapili mwaka huu ili kutoa nafasi kwa waamini wao kushiriki Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani kwa uhuru.

Monday, October 5, 2015

ULIMWENGU WA MACELEB: Unaweza kumruhusu binti yako wa miaka 14 atoboe pua?


Binti wa Jada na Will Smith, Willow mwenye miaka 14 ametoboa pua kama hivi. Wengi wetu kwa masikio sawa ila pua..mmh

Sunday, October 4, 2015

AY anataka mwanamke ambaye yuko smart kichwani

 ‘AY’ au Mzee wa Commercial ni mmoja kati ya wasanii ambao kwa muda mrefu sasa wako katika muziki wa kizazi kipya na amefanikiwa kujitunzia jina na ubora wa kazi zake unazidi kukua siku hadi siku.

Mchungaji Mtikila afariki katika ajali ya gari Chalinze



Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Chama Cha DP Mch Christopher Mtikila amefariki dunia kwa ajali ya gari kijiji iliyotokea cha Msolwa, Chalinze mkoani Pwani asubuhi ya leo na watu wengine watatu kujeruhiwa katika ajali.

Kingunge Mwiru ajitoa CCM....amesema hajiungi chama chochote ila anaunga mkono mabadiliko

Akizungumza kupitia vyombo vya habari Jumapili ya leo, mwanasiasa mkongwe katika Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali za chama na serikali ya Chama, Kingunge Ngombare Mwiru ametangaza rasmi hivi punde kujiengua uanachama ndani ya chama hicho.

Kingunge amesema ameamua kufanya hivyo kwa kuamini kuwa CCM haifanyi yale yaliyoasisiwa na kujengewa misingi bora na waasisi wa Chama. 
  
Aidha amesema hakusudii kujiunga na chama chochote cha siasa nchini. 

Akitathmimi anavyoiona hali ya sasa kisiasa nchini, amesema kila kundi katika jamii hivi sasa linataka mabadiliko. 


Saturday, October 3, 2015

Lowassa amtosa binti wa Sokoine....amwambia kama akitaka amfuate UKAWA laa amsamehe

MGOMBEA Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, ambaye anaungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), jana alitangaza kuitua mbeleko aliyokuwa akimbebea Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Monduli, Namelok Sokoine.

Regina Lowassa afafanua atakavyokuwa first lady.....Amesema ana uhakika mumewe atashinda

Mke wa Edward Lowassa ambaye ni mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Regina Lowassa, amesema ana uhakika mumewe atashinda katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu kutokana na muitikio mkubwa anaoupata katika mikutano yake na pia kiu ya wazi ya wananchi katika kufanya mabadiliko.

Kadhalika, ametaja vipaumbele vinne

Wednesday, September 30, 2015

Jinsi ya kutunza vyombo vya kupikia visivyong’ang’aniana na chakula (nonstick)


Vyombo vya kupikia visivyong’ang’aniana na chakula ni pamoja na masufuria na vikaangio. Vyombo hivi vina tabaka nyembamba ndani mwake linalofanya chombo husika kising’ang’aniane na chakula. Kwa kawaida kusafisha vyombo visivyong’ang’ania na chakula ni rahisi zaidi. Kiasi kidogo tu cha sabuni, sponji na maji ndivyo  unahitaji. Na baada ya hapo ni kuvifuta vizuri kabisa hasa kama maji unayotumia yana chembechembe za chumvi.
Zifuatazo ni dondoo za utunzaji wa vyombo vya aina hii.

Tuesday, September 22, 2015

Jinsi ya kuepuka mende ndani

Hakuna anayeweza kusimama na kusema anajisikia raha kuwa na mende ndani ya nyumba yake. Endapo mende wataingia ndani wanaweza kuharibu vyakula, vitabu, kusambaza magonjwa na hata kusababisha ukakasi machoni pale anapokuwa anakatiza.

Tuesday, September 15, 2015

Tabia 8 za watu ambao nyumba zao ni safi kila wakati

Hebu jiulize kidogo  kama mgeni akikutembelea bila taarifa unajisikia aibu kwa jinsi nyumba ilivyo. Kama ndiyo basi inaonekana una nyumba isiyokuwa safi kila wakati.
Fikiria ni kwa jinsi gani zaidi ungeweza kuwa na maisha ya raha kama ya watu wenye nyumba ambazo inachukua dakika 15 tu kuweka kila kitu sawa na hivyo nyumba yote kuonekana nadhifu.
Nimetafiti tabia za kila siku za watu  wenye nyumba safi

Friday, September 4, 2015

Vitu unavyoweza kuweka kwenye kabati la vyombo, zaidi ya vyombo

Tuseme una kabati lako la vyombo ambalo lina vipande viwili – kipande cha juu kikiwa na milango ya kioo na cha chini kikiwa na milango ilisiyoonyesha kilichomo ndani kwa mfano milango ya mbao au malighafi nyingine. Kwa kawaida sehemu ya chini ya kabati haina mvuto ila hii ya juu ndio inavutia.

Thursday, August 27, 2015

Unapoenda dukani kununua mapambo ya kiutamaduni fahamu dondoo hizi

Mandhari nzuri ya mapambo ndani ya nyumba ni ile ambayo inahakikisha umezungukwa na vitu na rangi ambazo unazipenda. Uwezo wa kuweka pamoja vitu hivi, kwa jinsi ambayo vileta muonekano wa kuvutia sio lazima iwe ni kitu cha kuzaliwa nacho.

Thursday, August 20, 2015

Dondoo za kufahamu kabla hujanunua taa za mezani

Taa za mezani ni muhimu kwa kila chumba  si tu kwa ajili ya  mwanga bali pia ni moja ya pambo la kuongeza rangi na staili. Kuzinunua inabidi kuwa makini ili usipoteze hela yako na muda vile vile. Hapa nimekuandalia dondoo unazopaswa kuzingatia wakati wa kufanya manunuzi.

Friday, August 7, 2015

Mke wa Dk. Slaa afunguka

Siku moja baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuzungumza na mwananchi na kusema yupo salama, mke wake, Josephine Mushumbusi amekanusha tuhuma zilizozagaa kuwa ndiye aliyemshauri kiongozi huyo wa Chadema kujiuzulu na kumzuia kushiriki vikao muhimu vya chama.

Thursday, August 6, 2015

Jinsi ya kupamba kwa vitu vyenye michoro kama iliyopo kwenye ngozi za wanyama


Michoro kama  iliyopo kwenye ngozi za wanyama haipitwi na wakati iwe ni kwenye nguo, vitupio na hata mapambo ya nyumbani.

Wednesday, August 5, 2015

Awesome!... Bibi miaka 89 anapokuwa mmoja wa bridemaids wa harusi ya mjukuu wake


At the dear old age of 89, Nana Betty is fast winning the heart of the nation after acting as her granddaughter’s bridesmaid.
Elizabeth Govern (or Nana Betty as her family call her) was asked by her granddaughter Christine to be one of her four bridesmaids because they’re BFFs and by the looks of things she stole the show.
Photos of the gorgeous granny have gone viral as she proved that being a bridesmaid shouldn’t just be left to the young ‘uns.

Monday, July 27, 2015

Bobbi Kristina, mtoto wa pekee wa Whitney Houston afariki dunia


Bobbi Kristina Brown ,mtoto wa marehemu Whitney Houston ambaye alikuwa gwiji wa muziki wa R&B ,amefariki dunia baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa miezi sita tangu alipokutwa taabani kwenye bafu lake na pindi alipofikishwa hospitalini na kukutwa na matatizo kwenye ubongo.

Friday, July 24, 2015

Jinsi ya kupamba nyumba yako kwa kuhusisha milango yote mitano ya fahamu

Msomaji wangu kichwa cha makala hii  ni kama vile kinakurudisha darasani! Je, unaikumbuka milango mitano ya fahamu? Mara nyingi tunasahau, wakati wa kupamba nyumba zetu tunazingatia mlango mmoja tu wa fahamu ambao ni macho. Ni vyema kuhusisha

Friday, July 17, 2015

Faida za bafu lenye bomba la mvua dhidi ya lile lenye sinki la kuogea


Karibu msomaji wangu kwenye makala ya leo ambapo tunaangalia faida za bafu lenye bomba la mvua dhidi ya lile lenye sinki la kuogea. Katika kuandaa makala hii nimefanya mahojiano na ndugu Rogers Mwenana ambaye ni muuzaji ma vifaa vya mabafu ya kisasa  kwenye duka moja katikati ya jiji la Dar es salaam.

Rogers anaanza kwa kutuambia kwamba

Tuesday, July 14, 2015

Mzee Yusuph amesema lazima aache muziki

Mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusuph amefunguka na kusema kuwa lazima aache muziki na kufanya kazi zingine nje ya muziki.

Monday, July 13, 2015

Kupenya kwa Dk Magufuli ni kama vita vya panzi furaha ya kunguru..mmh

Hatimaye Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha Dk. John Magufuli, kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Magufuli alipitishwa na CCM baada

Friday, July 10, 2015

Majina Matano CCM Ngoma bado Nzito


  • Mizengwe yatawala hadi usiku wa manane Kamati Kuu kufyeka waliodaiwa kuanza kampeni mapema.

Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imejikuta ikiwa katika kibarua kizito cha kuteua watia nia watano kati ya 38 wa nafasi ya urais mjini Dodoma jana usiku baada ya kuwapo kwa msuguano mkali juu ya watu wa kuwaondoa kwa tuhuma za kuanza kampeni mapema.

Wednesday, July 8, 2015

Wakati vikao vya juu vya CCM vya kuchuja wagombea urais vikianza leo, hofu na wasiwasi umezidi


Wakati vikao vya juu vya CCM vya kuchuja wagombea urais vikianza leo, hofu na wasiwasi umezidi kutanda miongoni mwa wagombea, viongozi na wanachama wa chama hicho kuhusu namna ya kuikabili minyukano baina ya wagombea hao na kibarua cha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Monday, July 6, 2015

AMUUA MKEWE MJAMZITO MIEZI 9 KWA WIVU...Marehemu apasuliwa na mtoto kukutwa kafia tumboni

MLINZI wa usiku katika Ofisi za Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Florence Kazonde (35) amejinyonga baada ya kumuua kikatili kwa kumkaba koo mkewe aliyekuwa na ujauzito wa miezi tisa, Emilia Mzui (30).

Sunday, July 5, 2015

ILANI YA UCHAGUZI CCM YAIVA..

KIKAO Maalumu cha Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza jana Mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Jakaya Kikwete, kwa ajili ya kupitisha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.

Amazing Pichaz..



Friday, July 3, 2015

AMEMUUA MWENZAKE WAKIGOMBEA MWANAMKE WA BAA

WATU watatu wamekufa katika matukio matatu tofauti katika Wilaya za Tarime na Rorya akiwemo mtu aliyeuawa wakati wanagombania mwanamke.

Kwanini tunapamba nyumba zetu?

Ni swali ambalo hatujiulizi sana lakini inabidi tujiulize. Ni vizuri tuwekane sawa kuwa tendo la kupamba nyumba ni la kibunifu na ni muhimu. Lina nia ya kuleta mpangilio kwenye maisha ili kujitoa kwenye mvurugano na machafuko ya jumla ya duniani, kuweza kuweka nguvu zetu za kupamba hata hapo padogo tunapoishi ambapo tuna uwezo napo.

Kwa kufanya hivyo tunaonyesha na