Utaijua bustani yenye afya wakati unapoiona: laini,
kama
vile ni zulia la kijani limetandikwa chini, ukitembea humo hamna majani makavu
yanayojaa miguuni kukufanya uchafuke miguu na viatu vyako. Sasa, kwa nini bustani
yako haionekani hivyo? Kupata muonekano maridhawa wa bustani huenda ikatakiwa
ubadili fikra zako, anasema mtaalamu na mbunifu wa bustani Hadija Adam. “Unajua
jinsi wanavyosema utamu wa ngoma uingie ucheze? Vyema, unatakiwa ugeuke ukoka.
Unatakiwa ufikiri ni nini ukoka unahitaji,” anasema Hadija.
Vitu vya msingi anasema ni vya kawaida
sana: jua, maji na mbolea.
Ukishapata hivyo hapo ni furaha tu - kwako na kwa bustani yako.
Kuanzisha bustani mpya ni mchakato wa raha na changamoto pamoja. Inabidi
maandalizi na mipango. Unatakiwa kuandaa eneo kwa kuondoa magugu yote na kujaza
udongo
kama itahitajika. Sasa hapa nikisema
kujaza udongo kumbuka sio kila udongo unafaa. Bi Adam anasema hatua ya muhimu
sana ambayo watu wengi
wanaruka ni hii ya kujaza udongo. Ni muhimu
sana kuweka udongo unaofaa na mbolea ya
ng’ombe (sio ya kuku kwa kuwa ina tindikali kali kwa hivyo haifai kwa kuoteshea
ukoka). Bi Hadija anashauri
kama kiasi cha
udongo ni robo tatu basi mbolea iwe robo. Katika kuchanganya na kusawazisha kwa
kureki usilazimishe
sana
tambarare fuatilia ardhi ilivyo na mwelekeo wa maji ili usijesababisha kuweka
dimbwi kwenye bustani yako wakati wa masika. Kuwa makini
sana kwa kuwa ukishaotesha ukoka wako
hutarudi nyuma tena na kuanza kung’oa kwa ajili ya makosa yaliyofanyika mwanzo.
Kuna aina
nyingi za ukoka (majani) unazoweza kuotesha kwenye bustani yako. Nyingine ni
laini na nyembamba sana
(fikiria uwanja wa golfu na wa mpira wa miguu), wakati ukoka nyingine unaweza
dhania umekanyaga nyasi kavu miguuni. Majani ni mengi na yanagundulika kila
mwaka. Kwa majani haya yote hali ya hewa inachangia unawiri wake.
Hakuna
swali ya kuwa kuweza kupata zulia zuri la ukoka lililofunga kila mahali kwa
wakati mmoja ni kwa kuotesha mbegu kila mahali wakati wa mwanzo. Lakini hii
inaweza kuwa gharama hasa kama unataka kufunga
eneo kubwa. Badala yake unaweza kununua mbegu chache ukaotesha kitaku nawe ukaanza
kujipatia mbegu zako kwenye kitalu hicho. Kumbuka hii ni kama kununua mbegu za
kuweza kutosha eneo lako ni gharama sana.
Kwa mfano, tukichukulia huu ukoka unaoitwa Canadian; mbegu za kujaa mfuko mmoja
wa saruji zinauzwa kati ya elfu 30-40. Sasa kama eneo lako utahitaji mbegu
mifuko hamsini kwa mfano, inaweza kuwa ni gharama kubwa kwako. Kwa hivyo nunua
mifuko michache uoteshe kitalu uvune mbegu mwenyewe.
Sasa
ukoka wako umeshaota na umeshafunga kila mahali na umerefuka kiasi ya kuwa
unahitaji kuukatia. Inapokuja kwenye swala la kukata ukoka wa bustani wenye nyumba
wengi wanashindwa kujua urefu sahihi. “Watu wengi wanakata ukoka wao kwa
kuuacha mfupi sana,
kitu ambacho kinayasababishia majani msongo,” anasema Bi Hadija. Anashauri
usetie mashine ya kukatia kwenye alama
ya juu kabisa. Majani yakibaki marefu yanafanya mizizi ikue vizuri na pia
inasaidia ardi isichomwe na jua la moja kwa moja na kuwa kavu kwani utaingia
gharama ya kuongeza umwagiliaji. Na usiamini kuwa ukiacha majani yawe marefu
ina maanisha kuyakata mara kwa mara kila baada ya muda mfupi, anasema Hadija. “Lakini
hii ni uongo kabisa "kuna upotofu kwa watu wengi kuwa
kama wakiyakata yakawa mafupi hautakata mara kwa mara,
huu ni uongo; yanaota haraka mno kiasi kwamba hayakupunguzii muda wowote wa
kukata tena.
Maji, maji, maji kila mahali. “Maji mara mbili kwa wiki ila
maji mengi” kwa Hadija hii ndio kanuni ya msingi. Maji ya kuzama yanasaidia
mizizi kupenya kina kirefu ardhini, wakati maji kidogo kidogo kila siku yanasababisha vishina
kukauka na kuzalisha majani makavu (ambayo ndio yanachafua miguu). Kumwagilia
kwa kina pia kunafukuza wadudu wanaojishika kwenye majani. Kwa bustani mpya
iliyooteshwa ukoka mwagilia maji mengi kila siku hadi mizizi ishike.
Bustani, hata ile unayoiona ina afya inahitaji chakula imara na hewa. Mara
mbili au tatu kwa mwaka wakati wa masika wataalam wanashauri ndio wakati wa
kuiwekea bustani mbolea. Kwa wakati huu mbolea ya kuku ndio inafaa zaidi hasa
kuweza kutunza ule ukijani wa ukoka unaohitaji.
Magugu kwaheri, sio ajabu kuwa karibia kila bustani itakuwa na magugu. Njia
nzuri ya kuangamiza magugu kwenye bustani ni kuchagua ukoka unaofunga kiasi
kwamba utayazuia magugu kushamiri. Yale machache yatakayopenya dawa yake ni
kuyang’oa.
Zingatia kanuni hizi za uanzishwaji na uendelezaji wa bustani na kila mmoja
atakuwa na furaha -- wewe na bustani yako.
Makala
hii imeandaliwa na Vivi O. Machange. Vivi ni mjasiriamali na ana mapenzi makubwa
juu ya muonekano wa makazi. Kwa maoni au maswali tuma kwenda 0755 200023 au
viviobed@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment