Hivi
ulishawahi kufikiria kuwa na makabati ya jikoni yenye rangi mbili tofauti? Yani
ya juu yawe na rangi yake na ya chini yawe na rangi yake tofauti.
Kutokana
na uwepo wa rangi nyingi za finishing za makabati ya jikoni, baadhi ya wenye
nyumba na wenye nyumba watarajiwa wanafikiria kuchanganya rangi mbili kwa ajili
ya makabati ya jikoni. Mtindo huu unakuja kwa kasi kadri nilivyoongea na
mseremala Andrew Komba wa kampuni ya kutengeneza fenicha ya Furniture Mart
iliyopo Tabata Dar es Salaam. Anasema makabati haya yanaonekana ya kisasa na kufanya
jiko lipendeze.
Iwe
ni kwa muonekano au kuficha makosa yaliyojitokeza kwenye kupendezesha jiko,
kuna sababu nyingi za
kuwa na makabati ya jikoni yenye rangi mbili tofauti. Kama
unatafuta njia ya kuongeza rangi,
unaweza kufikiria kuwa na makabati yenye rangi mbili tofauti. Mtindo huu ni mzuri
kutengeneza kitovu cha jiko hasa endapo halina kisiwa (mfano wa kauta ndogo ya
katikati ya majiko ya kisasa). Kwa majiko yenye kisiwa kwa vile kiko kati
kinaweza kuwa ndio kitovu cha jiko.
Muonekano
wa jiko ni muhimu kwenye kuleta mvuto. Makabati ya jikoni ya rangi mbili yanakupa
wigo mpana wa kubuni jiko lako huku ukihusisha rangi za kuta, kaunta, sakafu na
mlango. Pia ni njia nzuri ya kufikia muafaka kama hamuwezi kukubaliana rangi za
makabati ya jiko na mwenza wako!
Makabati
ya jikoni yenye rangi mbili tofauti (zilizo sahihi) yanasaidia jiko lionekane
kubwa. Kwa mfano, jiko dogo lenye dirisha lililoelekea eneo ambalo mwanga wa
jua ni kidogo, makabati yenye rangi
nyepesi yatafaa zaidi kuliko ya rangi nzito kwa ajili rangi hizi zinafanya jiko
lionekane kuwa na mwanga na kubwa.
Vivyo
hivyo, rangi nzito zinapendeza kwa makabati ya chini huku yale ya juu yakiwa na
rangi nyepesi. Mtindo huu una faida
kadhaa ambazo ni pamoja na kulifanya jiko lisionekane kujaa na vilevile
kutengeneza hisia za eneo kuwa kubwa
kuliko lilivyo. Vile vile haya ya chini yenye rangi nzito yanalipa jiko hisia
za kinyumbani zaidi.
Mtindo
wa kupaka makabati ya juu rangi nzito na ya chini nyepesi haujapendelewa na
wengi wenye kutaka kabati za rangi mbili. Ila faida yake ni kwamba makabati ya
juu ya rangi nzito yanaleta hisia ya dari kuwa chini hivyo kuweza kuonyesha zaidi
ubunifu wa usanifu wake.
Endao
unataka kupaka makabati ya jikoni rangi mbili tofauti unapaswa kuhakikisha kuwa
rangi hizo zinaendana na za maeneo mengine ya jiko.
Mwishoni
kabisa kumbuka kuwa endao unapaka makabati rangi mbili tofauti itapendeza
kaunta zikiwa nyeupe au krimu laa sivyo zikiwa nazo ni ya rangirangi jiko
linaweza kuonekana halijatulia kwani makabati na kauta viko jirani mno.
No comments:
Post a Comment