Chumba
kilichokamilika kina kuta, mlango, dari na dirisha. Kwenye makala hii
tunaangalia vitu vinavyohitajika ndani ya chumba kamili cha kulala.
Chumba
chako cha kulala ndio sehemu yako takatifu, je kwanini
usihakikishe kina vitu
hivi?
1.
Kitanda na matandiko
Kimsingi vitu hivi ndivyo vimefanya
chumba hiki kiitwe ni cha kulala.
2.
Zulia
Hakuna
sakafu inayoweza kuburudisha miguu peku unapotoka kuamka asubuhi kuliko ya
zulia. Jipendelee kwa kuhakikisha kuwa hatua yako ya mwanzo wa siku ni ya
burudani. Hata kama huwezi kununua zulia la kutosha chumba kizima basi weka
japo dogo la pembeni kwa kitanda.
3.
Mito ya kutosha
Kulingana na ukubwa wa kitanda
chako, idadi sahihi ya mito ni miwili hadi sita. Kitanda kiwe na mito ya
kulalia pamoja na ile ya mapambo. Na pia muundo wa mito ya mapambo waweza kuwa wowote kama
vile pembe nne, soseji na moyo. Kwa kulalia, mito inayofaa zaidi ni ya pembe
nne.
4.
Eneo la kukaa (ambalo sio kitandani)
Eneo la kukaa linakusaidia wakati wa
kusoma au wa mazungumzo na mwenzi wako. Pia ni pazuri kunyanyulia mguu wakati
wa kuvaa soksi. Vilevile unapotandua matandiko kwa ajili ya kulala
unahitaji kuondoa na kihifadhi vile vitu
ulivyopambia kitanda kama vile mito, utepe wa kitanda na shuka au duveti la
mapambo. Ingawa kwa baridi inabidi utumie huu uzinduzi wa Ulaya (duveti)
kujifunikia. Eneo la kukalia kwenye chumba cha kulala linakusaidia kuhifadhi
vitu hivi (kwa ajili ya kuvitandika kesho yake) badala ya kuviweka chini.
5.
Sanaa na picha unayoipenda
Haimaanishi kwamba chumba kiwe na
mrundikano wa picha na sanaa ila unapoweka vitu vichache unavyovipenda eneo
unaloviona kwa muda mrefu ni kwamba inazidisha furaha yako. Unapokuwa na furaha
unapata usingizi mzuri na unaanza siku kwa furaha.
6.
Taa za vivuli kila upande wa kitanda
Kuna wakati ukiwa umelala unajisikia
kusoma kitabu, jarida au gazeti. Ili usimsumbue wa pembeni yako kwa mwanga
asiohitaji, kutumia taa ya kivuli iliyo upande wako ndio suluhisho. Zaidi ni
kwamba taa hizi ni sehemu ya kupendezesha chumba.
7.
Pazia
Chumba cha kulala si kama cha
jikoni. Kinahitaji faragha na hisia za giza hata kiwe ni cha rangi za mwanga
kiasi gani. Weka pazia sahihi.
Namaliazia
kwa kukuuliza swali msomaji wangu, je chumba chako kina vingapi kati ya hivi?
No comments:
Post a Comment