Kununua ardhi na kutaka kuanza kujenga nyumba yako bila
shaka ni hisia nzuri. Je, kuna kitu kizuri zaidi ya kubuni na kupamba nyumba
yako mwenyewe?
Bila shaka hamna! Ukimiliki nyumba unajisikia ni kama
huhitaji kitu kingine zaidi katika maisha yako. Mahitaji makuu ya msingi ya
binadamu ambayo ni chakula, mavazi na
malazi yanapatikana pale ambapo kuna
nyumba.
Lakini kuna kitu unachotakiwa ujue kwamba pale unapotaka
kujenga nyumba ni muhimu kuwa na ramani inayotoka kwa msanifu wa jengo.
Unajiuliza
kwanini? Msanifu wa majengo kazi yake ni kuchukua mawazo yako wewe unayetaka
kujenga na kuyabadilisha kuwa mchoro unaokubalika kwenye ujenzi. Bwana David Sembuyagi
ambaye ni msanifu wa majengo anatupa faida za kumshirikisha msanifu ili
akuchoree ramani kabla ya kujenga nyumba
.
Sio rahisi wewe unayetaka kumiliki nyumba kuweza kuibuni
mwenyewe - Kuna vitu vingi vidogo na vikubwa ambavyo unapaswa kuvitilia maanani.
Hata kama una kipaji cha ubunifu, bado unahitaji mtu ambaye anaweza kukuchorea
ramani ya nyumba nzima kitaalam. Kumbuka kitu kimoja, ni gharama kubwa mno na
pengine huwezi kuja kuvunja nyumba nzima kwa ajili uliijenga vibaya!
Mtaalam huwa anatumia uzoefu wake - Kama uko kwenye nyanja
nyingine hutegemewi kuweza kusanifu ramani ya nyumba kitaalama kwa namna ambapo
msanifu mtaalam angefanya. Ana uzoefu wa kutosha na uwezo wa kufanya kazi yako
bila wewe kuwa na wasiwasi wowote ambapo
itakusaidia kupunguza msongo wa mawazo mbeleni!
Huwa gharama zao sio kubwa sana, kama ndio wasiwasi wako
- Labda uwe muflisi kabisa, vinginevyo una gharama kidogo ya kulipa kwa ajili
ya ramani. Habari njema ni kwamba baadhi ya hawa wataalam wako tayari
kukufanyika kazi yako kwa bei ya makubaliano.
Kama hutaki msanifu akuchoree ramani basi walau mwache
akuongoze -Kuna baadhi ya watu ambao ni wasumbufu kiasi kwamba wanaweza kubuni
nyumba nzima peke yao. Kama wewe ni mmoja wao, mtumie msanifu akuongoze kwa
jambo hilohilo. Mpe nafasi atumie utaalam wake kukuwezesha kupata nyumba
sahihi.
Unapata mtu wa kumshirkisha ndoto yako - Ile tu msanifu
kukusikiliza, halafu kukubunia ramani, inakupa hali ya kujiamini!
Mwisho kabisa ni
kwamba kisheria unapoanza ujenzi unatakiwa kuwa na kibali. Kibali hakipatikani
bila kuwa na ramani ya jengo.
Vivi ni mshauri wa mapambo ya nyumba. Je kuna lolote linakutatiza kuhusu namna ya kupendezesha nyumba yako? Nijulishe 0755 200023
Nifuate instagram: vivimachangehomes
No comments:
Post a Comment