Tunaweza kusema kuwa wallpaper ndio habari ya mjini kwa sasa
kwa ajili ya kupendezesha vyumbani kwenye nyumba nyingi za kisasa hasa chumba
che sebule. Tatizo lililopo ni changamoto ya mtindo upi ndio sahih kutokana na
uwepo wa wallpaper za rangi na michoro mingi mno. Hadi zile flati yaani zisizo
na mchoro wowote.
Nimehojiana na Bi Phides wa Phides Décor kama mtaalam wa
wallpaper ili kupata dondoo zake za ni kwa namna gani mnunuzi anayetaka kupamba
kwa pambo hili anavyoweza kununua ya mtindo sahihi kwa chumba sahihi.
Anasema
pale unapokuwa umefikia uamuzi wa kwamba unataka kupendezesha chumba fulani kwa
wallpaper kuna maswali kadhaa ya mitindo ya
wallpaper unatakiwa uweze kujijibu.
Je chaguo zuri kwako ni wallpaper yenye michoro au iliyo flati? Jibu hapa
linategemea na ladha binafsi ya mwenye kutaka kupamba. Wallpaper yenye michoro
hata kama ni ya rangi sawa na ya wallpaper yenyewe, kwa kawaida inasaidia
kuficha makosa yoyote yaliyopo ukutani.
Wallpaper flati inakupa wigo mpana
wa muonekano wa kung’aa na metaliki.
Lakini kwa ujumla mimi Phides kama mpambaji na muuzaji wa wallpaper nimeona
wateja wangu wengi zaidi wakipendelea wallpaper zenye michoro kuliko zile za
flati.
Zingatia kiasi cha mwanga kwenye chumba
husika. Pata jibu kuwa je chumba hicho kinahitaji wallpaper ya rangi nzito au
nyepesi ili kiwango cha mwanga kisiathirike iwe ni
asubuhi, mchana au usiku.
Je ni ukuta wa
chumba gani unaotaka kuubandika wallpaper?
-Kama ni
chumba cha kulala cha wanandoa, wallpapaer zenye maua ndiyo inafaa zaidi kwani
inaleta hisia ya mahaba.
-Kama ni
sebule yenye mapambo ya mtindo wa kisasa (rejea makala ya mitindo minne za
kupamba ndani), wallpaper yenye michoro ya rangi nzito, metaliki, ya kung’aa na
ya mguso wa mtelezo ndio inafaa zaidi
kwani ndiyo inayoonekana ni za kifahari.
Swali lingine
la kujiuliza upate majibu ni kwamba je ni kwa staili gani unataka kubandika
hiyo wallpaper yako. Staili zote hazileti muonekano unaofanana, sawa eeh? Kwa
mfano kubandika wallpaper kwenye ukuta mmoja tu kati ya nne za chumba sio sawa
na kubandika kwenye kuta zote nne. Chagua wallpaper yenye rangi nzito kama
unabandika kwenye ukuta mmoja tu kwa mfano ule wa luninga kwa sebuleni au wa
tendego kama ni chumba cha kulala. Staili ya wallpaper yenye rangi za namna
hiyo, metaliki na mtelezo itatoa muonekano wa kiwango na kuvutia. Vilevile
wallpaper za mtindo huu zinapendeza pia kwenye dari.
Chumba
kidogo kinapendeza kikibandikwa wallpaper isiyo na michoro au maua laa kama
inayo basi yawe ni yale madogodogo. Wakati huohuo chumba kikubwa kikipendeza kwa
wallpaper yenye michoro na maua makubwa.
Kwahivyo ukishakuwa na vigezo hivi
kichwani, ni rahisi kwako kwenda dukani na kuchagua wallpaper sahihi.
No comments:
Post a Comment