Tumia
mito ya sakafuni kwa kukalia na kama pambo
Mto wa sakafuni ni
kusheni kubwa linalotumika sakafuni kama pambo au mahala pa kukalia. Mto huu
huwa umejazwa zaidi na ni mgumu kuliko mito ya kawaida ya kwenye sofa ili
kuweza kuhimili uzito wa mwili. Mara nyingi mito hii ni mikubwa na hutumika
kukalia wakati wa burudani kama vile wakati wa kutazama luninga na pia ni nyongeza ya mahali pa
kukalia kwenye vyumba vya michezo ya watoto.
Mto wa sakafuni unaweza
kuwa na umbo lolote liwe ni duara, boksi ama mraba. Weka mito yako mitatu juu
ya kizulia chako cha kutupia na mara utagundua kuwa umetengeneza sehemu ya
nyongeza ya kukalia wakati wa burudani au mahali poa pa kusoma na kustarehe.
Chagua mito ambayo itaendana na kizulia chako. Mpangilio wa kizulia hicho na
mito yenye rangi za kukolea utaleta mvuto. Pia unaweza kupendezesha sakafu yako
ya marumaru au mbao kwa kutupia mito ya sakafuni. Chagua rangi za ladha yako
kuendana na rangi ya sakafu ili kuleta muonekano wa mapambo ya kisasa.
Mito ya sakafuni ni pambo
rahisi ambalo kila nyumba inaweza kuwa nalo. Kama wazo lako la mito ni kuweka
kwenye sofa tu; basi unahitaji kuchukua
muonekano mwingine. Mito hii inakuja kwa saizi mbalimbali kwa jinsi ambayo
inaweza kumfurahisha kila mtumiaji awe ni mtoto, kijana ama mtu mzima. Unakutana
na matumizi mengi ya mito mikubwa ya sakafuni na utashangaa ni kwa vipi unaweza
kuishi bila hiyo. Hata kwa kukaa tu na kutulia kutafakari maisha au kucheza
karata karibu na meza ya kahawa, mito ya sakafuni inafanya kukaa sakafuni kuwa
ni raha na shughuli zako kuwa za starehe zaidi
Watoto wanaipenda! Ni
muhimu wakati wa kucheza na watoto. Ukiwa unakaa karibu na watoto mara kwa mara
utaanza kugundua ni muda mwingi kiasi gani wanaoutumia sakafuni. Na pia ni muda mwingi kiasi gani wanapenda
ukae nao hapo sakafuni! Kama una mtoto mdogo utakugundua kuwa mto mkubwa wa
sakafuni ni sehemu tosha kwa usingizi kwa mchana.
Pia kwa swala la
usalama, watoto wadogo hawako makini kihivyo; na hasa wanapokuwa wanakimbia na
kuishia kujirusha kwenye sofa. Ndio hapo wapohitaji mto mkubwa wa sakafuni
kuangukia. Na hata wanapong’ang’ania kubembea kwenye mikono yako hadi
unaposikia kama mikono inataka kung’oka, basi sehemu ya kuwatulizia ni kwenye
mito ya sakafuni.
Kwa kuhurumia magoti
yako idadi ya mito inavyoongezeka ndio na uzuri wake unavyoongezeka.
Kwa nini
ukae tu juu ya kizulia uumizwe na sakafu wakati kuna mto mkubwa wa kunesa ambao
ungeweza kuukalia? Wakati familia yako ikiendelea kukua na sehemu ya kuweka
fenicha imeshajaa, mito mikubwa ya sakafuni ni mbadala tosha wa viti. Kwa
mikutano ya familia na marafiki wakati ambapo hamna viti vya kutosha hufurahii
wale wanaoshia kukaa sakafuni wapate starehe (hata kama ni watoto?)
Mito ya sakafuni
inayokunjika ni chaguo zuri. Hii ina sehemu tatu, kunjua wote kama unataka
kulala kwa tumbo; halafu kama unataka kukaa kwa muda; ukunje zile sehemu mbili
ili usaidie mgongo na sehemu ya tatu kalia. Mito ya aina hii pia ipo ya
kufanana kama fenicha kabisa ambayo ina hadi sehemu za kupumzisha mikono.
Je una kimnuso cha binti yako mdogo
nyumbani? Ni nini kinachoweza kuwa rahisi zaidi ya kuweka nusu dazeni ya mito
hii kwenye sakafu ya sebule yako. Wacha waangalie katuni hadi wasinzie halafu
waache hapo, ukijua kuwa wana kitanda na mto pamoja! Kwa hivyo kama isivyo kwa
mapambo mengine ya ndani, mito ya sakafuni inawekwa kwenye matumizi ya kukalia na
mapambo kwa wakati mmoja.
Mito ya sakafuni inaweza kuwa kwenye
kitambaa chochote utakacho hadi kwenye ngozi na hata plastiki kwa ajili ya ile
ya kwenye varanda. Baadhi ya watu wanapenda kuoda mito ili watengenezewe
kuendana na mapambo yao mengine ya ndani au hata mapambo ya chumba husika. Ingawa
hii inaweza kuwa gharama zaidi lakini inakuwezesha kupata foronya za rangi
upendayo na utakazoweza kubadilisha kadri upendavyo.
Kama unataka kuburudisha nje ya
nyumba kwenye varanda yako tafuta mito ya sakafuni ya nje. Mito hii ya sakafuni
ya kwenye varanda inatengenezwa kwa foronya za kudumu kwa mfano za kanvasi, ngozi
ama plastiki, ili kujikinga na unyevu maji na hata kuzuia kupauka kirahisi.
Wakati usioihitaji ihifadhi stoo ili kuiwezesha idumu.
Mito ya sakafuni inatumika kama
pambo na mahali pa kukaa pale ambapo urefu wa kiti ama usaidizi wa kina wa
mgongo hauhitajiki. Kama unavyoweza kuona, jinsi ambavyo mto wa sakafuni
unavyoweza kutumika kama pambo au kama fenicha nyumbani kwako ubunifu tu ndio
unahitajika. Wageni wako watu wazima wanaweza kuunganisha mito ya sakafuni
kadhaa wakavuta shuka na tayari kuwa kitanda bandia cha mgeni Kwa hivyo unasubiri nini kuwa na
mito ya sakafuni?
Makala hii imeandaliwa na Vivi O. Machange. Vivi
anajishughulisha na usafi wa mazulia na nguo aina zote; pia ana mapenzi makubwa
ya mitindo na mapambo ya nyumbani. Kwa maoni au maswali tuma kwenda viviobed@yahoo.co.uk au 0755 200023
No comments:
Post a Comment