Pendezesha
bufuni kwako kwa kuweka vizulia
Ni wachache wetu wanatumia muda wao wa thamani
kuweka mazingira yenye kuleta mvuto na burudiko bafuni. Unaweza kuweka vizulia
vya bafuni kwa matumizi na pia kama
mapambo kuongeza ufahari wa muonekano wa bafu zako. Bafu nyingi zina sakafu za
marumaru ambayo inaonekana maridadi sana lakini inaweza kuwa baridi kwa vidole
vya miguu mitupu. Vizulia vya bafuni zaidi ya kuwa mapambo ni burudani kwa
miguu yako.
Vizulia vya bafuni vinaweza kusaidia sakafu ya bafu
kuwa na hisia ya joto na mvuto kwa watu waliopo ndani ya nyumba. Vizulia vingi
vya bafuni havitelezi na vinatumiwa sana bafuni kuruhusu watoto na
wazee kujikinga na sakafu ya baridi.
Vizulia vya bafuni ni njia rahisi kuliko zote za
kuleta muonekano maridadi bafuni. Wala hutakiwi kupaka rangi upya au kuweka
marumaru mpya ili kuleta muonekano mpya bafuni. Wewe weka tu vizulia sahihi na
vitupio kadhaa na kila mtu atadhani kuwa umejenga upya bafu zako.
Unaweza kupata vizulia lukuki ambavyo vitakufaa kwa
matumizi ya bafuni. Ila kwa kawaida huwa vizulia vya bafuni vinakuja kwa seti
yake lakini hii haikuzuii kuwa mbunifu kwa kuweka vizulia bafuni kwa ladha
yako.
Huna haja ya kung’ang’ania vizulia
vya umbo la yai na duara ambavyo vimezoeleka na wengi kuwa ndivyo vya bafuni.
Wakati wa kuchagua vizulia vya bafuni ni muhimu
kuzingatia kuwa bafuni ni muhimu kama vilivyo vyumba vingine vilivyo ndani ya
nyumba yako. Kwa hiyo chukua muda kufikia maamuzi juu ya ni muonekano gani
unataka kuujenga bafuni. Kwahivyo moja kwa moja utachagua vizulia sahihi kwa
kuhuisha mapambo yako ya bafuni.
Seti za vizulia vya bafuni ni gharama nafuu kwa mtu
wa maisha ya kati na kuna aina mbalimbali kwa mhusika kuchagua. Kama wakati wa
kuchagua sakafu ya kuweka kwenye nyumba unavyohitaji iwe imara, vilevile kabla
ya kununua vizulia vya bafuni hakikisha kuwa vinadumu, vinaweza kustahimili mazingira ya bafuni, ni
rafiki kwa watoto, vinaonekanaje na unavihisije ukiwa na umevikanyaga kwa miguu
mitupu.
Sakafu ya bafuni huwa inapata matone ya maji ambapo
inaweza kusababisha utelezi. Vizulia vya bafuni vinakupa kituo cha kusimama kwa
kujiamini kuwa hutaanguka pale unapotoka kwenye sinki au bomba la mvua la kuongea.
Vizulia vya bafuni vinatakiwa viwe vinavyosafishika
kirahisi . Havitakiwi kuwa na unyevu nyevu unaotokana na maji ya moto ya
bafuni. Vile vizulia vyenye mpira kwa chini ni sahihi kuzuia uozo na kuvujisha
maji. Hata hivyo jua kuwa vizulia vitatakiwa kuanikwa mara kwa mara kufanya
tatizo la unyevu na uozo lisiwepo.
Vizulia vya bafuni mara nyingi vinawekwa yale maeneo
yanayoweza kuloa maji kirahisi. Maeneo hayo hasa ni kama pale kwenye eneo la
kuogea na la kunawia mikono. Pia
vinaweza kuwekwa kama tandiko la mlango wa bafuni. Ukubwa wa bafu ndio utaamua
kama uweke kizulia kikubwa au vingi vidogodogo.
Ingawa kulikuwa na hasara kadhaa za kuweka vizulia
bafuni, watengeneza mazulia wamechukua hatua madhubuti dhidi ya malalamiko
makuu kuhusu zulia za bafuni – unyevu, ukungu na madoa. Ni rahisi kubadilisha
zulia kuliko kubadilisha sakafu iliyooza.
Baadhi ya njia za kawaida ambazo vizulia vinaweza
kukutana na unyevu bafuni ni pamoja na bakteria wanaojazana kwenye lile eneo la
kuzunguka sinki la choo. Bakteria wanaokuwa kwenye mkojo kwa bahati mbaya
wanaweza kusambaa kwenye zulia. Safisha vizulia mara kwa mara kuondoa ukungu na
bakteria wanaoweza kuwepo. Hakikisha mara zote vizulia ni vikavu iwezekanavyo.
Pia kuna vifaa mbalimbali vinavyoweza kusaidia kuzuia maji yasipite kwenye
pazia la bafuni na kurukia kwenye kizulia.
Ingawa kizulia chochote kinaweza kutandikwa kwenye
sakafu ya bafuni, ambavyo vinatumika
sana ni vile vizulia vya bafuni vyenye mpira kwa chini. Faida ya zulia za
bafuni ni kuwa zinafanya bafu lionekane maridadi na lenye mvuto. Ni vilaini
kuliko marumaru kwa hivyo watu wengi wanaburudika kuvikanyaga na miguu
mitupu. Ajali za kuteleza bafuni
zinapungua. Ni rahisi kuteleza kwenye
sakafu ngumu ya bafauni kama vile marumaru kuliko kwenye zulia.
Kumbuka mapambo mengine hapo bafuni. Fikiria mwanga
wa taa na rangi ya sakafu na vifaa vingine vya usafi vilivyopo hapo bafuni. Vizulia
vya rangi za kung’aa vinafaa kwenye bafu
za watoto na vinaleta mvuto sana sakafuni.
Kwahivyo kama unataka macho yaelekee kwenye vitu vingine kama kioo cha
ukutani weka vizulia vya bafuni visivyokuwa na rangi kali. Staili na mandhari
mbalimbali zinaweza kupatikana mitandaoni au kwenye majarida ya mapambo ya
ndani.
Kwa hivyo kama unataka kuweka muonekano mpya wa bafu
lako vizulia ni chaguo sahihi na gharama nafuu zaidi. Vizulia sahihi vya bafuni
vitafanya bafuni kuwe sehemu ya burudani kwa watoto. Ulishapata ugeni wa watoto
nyumbani na wakawa hawaishi kuomba kwenye bafuni? Ni kwa kuwa kunavutia! Hebu
fikiria umeweka vizulia vyenye katuni za spiderman, pazia la bafuni na miswaki
inayooana, hutakaa ugombane tena na watoto wako wadogo kuhusu kupiga mswaki na
kuoga. Vizulia visiwekwe kwenye bafu za jumuiya!
Makala hii imeandaliwa na Vivi O. Machange. Vivi
anajishughulisha na usafi wa mazulia na nguo aina zote; pia ana mapenzi makubwa
ya mitindo na mapambo ya nyumbani. Kwa maoni au maswali tuma kwenda
viviobed@yahoo.co.uk au 0755 200023
No comments:
Post a Comment