Wednesday, October 21, 2015

Faida za kuwa na kioo juu ya meza ya chakula ya mbao


Meza ya chakula sio tu sehemu ya kukutana familia na marafiki wakati wa chakula, bali pia ni fenicha kubwa yenye kuhusika na muonekano wa ndani. Kama umeshanunua moja au labda unayo tayari bila shaka utakuwa nayo maisha yako yote. Kwahivyo fanya kila uwezalo ili kuiwezesha ivutie na idumu miaka mingi.

Pamoja na kuwepo kwa meza za
chakula za aina mbalimbali, makala hii itakurahisishia kujua faida ya ile ya mbao lakini yenye kioo juu yake. Kioo hicho aidha unaweza kuwa umekinunua moja kwa moja na meza yake ama umekitengenezesha kuendana na muuondo wa meza yako.

Kwanza kabisa lazima tukubaliane kuwa meza sahihi unayoweza kuweka kioo juu yake ni ile iliyotengenezwa kwa mbao ngumu kama vile mninga mkongo na mahogany. Meza ya mbao ngumu hata inapowekewa kioo cha uzito mnene (ambacho ndicho kinatakiwa) huna wasiwasi kuwa itaporomoka. Meza nyingine za mbao laini au mabaki ya mbao zinaweza kukuridhisha tu kiuchumi na muonekano lakini si kitu cha kudumu.

 Kwa kawaida kioo ni njia mojawapo ya kutengeneza hisia za ukubwa wa eneo. Kwahivyo endapo chumba cha chakula ni kidogo, kuweka kioo juu yake inakupa faida ya kuakisi mwanga na chumba kuonekana ni kikubwa. Na hata kama umebahatika kuwa na chumba kikubwa, muonekano wa kioo juu ya meza unaleta umaridadi, mng’ao na fahari ndani ya chumba.
Pia kioo juu ya meza ni moja ya mapambo ya ndani na kinaifanya meza kuwa kwenye fasheni isiyopitwa na wakati kwa kuonekana mpya kila siku.

Kioo juu ya meza kinasaidia kulinda mbao iliyopo chini yake. Hivi vioo huwa ni vigumu, ambapo inamaanisha hakiwezi kukwaruzika na si cha kuparaganyka kama kikigogwa. Pia vioo mahususi kwa ajili ya meza vina kiwango vyake vya usalama kwa hivyo kama kioo hakijaja na meza tafadhali usitengenezeshe kienyeji shirikisha mtaalam.

Faida nyingine ya kuwa na meza ya chakula ya mbao yenye kioo juu ni kuwa huna haja ya kitambaa cha meza. Na pia utunzaji wa meza hii ni rahisi sana. Unaweza kuifuta bila kuogopa vyakula na majimaji yatabaki yamesimama mezani.


Vivi ni mshauri wa mapambo ya nyumba. Kwa maoni au maswali tembelea www.vivimachange.blogspot.com

No comments:

Post a Comment