Jinsi ya kutengeneza na umuhimu wa eneo la kuingia kwenye
bustani
Eneo la kuingia kwenye bustani ya
maua ni kiungo muhimu cha bustani ya nyumba yako. Ni eneo sahihi la wewe mwenye
bustani kuonyesha ladha na ubunifu wako binafsi.
Muonekano wa kuvutia wa eneo hili
sio tu unaboresha muonekano wa bustani bali pia ni ishara kwa wageni wako kuwa
wameshafika bustanini. Eneo hili ni kama
linasema“hapa ndio mahali panapoanzia bustani yangu ya nyumbani,” anasema
mbunifu wa bustani Bi Tatu Mbegu.
Kuna staili nyingi tofauti za eneo la
kuingia kwenye bustani au sehemu nyingine ya nje ya nyumba. Katika makala hii
mbunifu Tatu Mbegu anakushauri aina hizi mbalimbali na ndipo utakapoweza kuamua
ni ipi itafaa kwenye bustani yako.
Sehemu ya kuingia kwenye bustani inaweza kuwa eneo rahisi tu kwa mfano mawe mawili yaliyowekwa mkabala katika eneo hilo, vyungu vya maua, kiingilio kama fremu ya mlango kwa mfano wa vibao vya kupishana au hata chuma, milingoti miwili iliyozungushiwa mimea mitambaazi na hata geti la chuma na kadhalika na kadhalika. Uwezekano ni mwingi na upeo ni mwisho wa ubunifu wako. Vizuri, kitu muhimu cha kufahamu ni kuwa ni eneo la mwanzo linaloonekana kabla ya kuingia kwenye bustani, anasema Tatu. Eneo hili linatoa tamko la papo kwa papo la utambulisho wa mwenye bustani na linaleta mguso wa eneo lingine lote la bustani lililobakia.

Mbao na chuma zinaweza kuchanganywa
kwa uzuri na kufanya eneo la kuingia. Vifaa vya ujenzi navyo vinafanya wigo
mpana wa kuchagua mtindo wa muonekano wa eneo hilo. Kama unadhani mbao
zinaonekana kuoza sana ndani ya muda mfupi basi tumia chuma peke yake.
Pamoja na hayo ni muhimu kufahamu
kuwa sio kila eneo la kuingia kwenye bustani liko mbele ya nyumba. Wengine
hupendela kugawa bustani kwenye vyumba na hivyo kuwa na maeneo tofauti ya
kuingia katika kila chumba.
Kuzungushia hiyo fremu ya eneo la kuingia
kwa mimea na maua inaonyesha ubunifu zaidi. Mgeni anayepita chini ya kivuli anafunikwa
na kijani na hivyo kujisikia burudani kwa hewa safi.
Hii yote inatokana na ladha ya
mwenye nyumba, muonekano na bajeti. Eneo la kuvutia la kuingia kwenye bustani
ni utambulisho wako kwa mapambo yako ya nyumbani.
Sasa unaanzaje kupata mawazo ya jinsi ya kutengeneza eneo la kuingia? Bi Tatu anajibu swali hili kwa kusema kuwa anza kubuni kwa kuangalia kwanza bustani yako kwa ujumla. Ni wapi ungependa kuweka eneo la kuingilia? Wakati mwingine uamuzi unatokana na eneo lililozoeleka kupitwa hapo kabla, na pia ni jinsi gani ungependa wageni waifikie nyumba yako? Je unapenda kubuni njia ya moja kwa moja kutoka kwenye bustani kuingia kwenye nyumba ama kuwe na kona ya kuingia kwenye bustani kwanza kabla ya kufikia mlango wa mbele wa nyumba?

Halafu jifanye kama wewe ni mgeni
kwenye makazi yako mwenyewe. Jiulize kama ungefika mahali hapo kwa mara ya kwanza
ni wapi ungepitia kufika bustanini. Sasa weka baadhi ya maelezo haya kwenye
mawazo yako ya kuamua ni wapi utengeneze sehemu ya kuingia kwenye bustani yako.
Hakikisha kuwa utatumia njia yako ya
kuingilia kwenye bustani. Hii ina maana kuwa kama utaitengeneza mahali ambapo
huvutiwi kupitia basi ni dhahiri kuwa utaitumia kwa mara chache sana au hata
inawezekana hutaitumia kabisa. Kwa hiyo kabla hujatengeneza njia hakikisha kuwa
utaitumia.
Muonekano wa eneo la kuingilia uwe
ni muendelezo wa mapambo mengine ya nyumba yako. Kama nafasi inaruhusu
tengeneza eneo la kutosha kwa ajili ya kupitia watu kadhaa. Eneo la kuingilia
la upana mdogo zaidi ni mita moja na nusu kwa bustani ya wastani hadi mita
mbili na nusu kwa bustani kubwa, anasema Bi Tatu.
Mwisho fikiria bajeti; haihitaji
hela nyingi kutengeneza eneo la kuingia kwenye bustani. Kama mbunifu alivyosema
kuwa hata vyungu viwili vilivyooteshwa maua vikawekwa mkabala vinaweza kufanya
eneo la kuingia kwenye bustani, au hata boda za maua zilizozunguka bustani zinaweza
kuachwa nafasi ya eneo la kuingilia na ikawa ndio hicho tu unachohitaji. Ni
rahisi tu kama hivyo wala haihitaji mambo makubwa.
Wawezeshe wageni wako kupunguza
mwendo wanapofikia bustani yako kwa kuweka njia ya kuingilia, watafurahia kwa
undani maua mazuri na mimea laini ya bustani yako.
Makala hii imeandaliwa na Vivi Machange ambaye ana mapenzi makubwa juu
ya muonekano wa makazi. Kwa maoni au maswali tuma kwenda 0755 200023 au
viviobed@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment