Kumpenda mwingine, ni muhimu kujipenda mwenyewe kwanza. Mtu
anatakiwa kujithamini utu wake mwenyewe na kujifurahia alivyo. Kila mmoja
anajiona mzuri mbele ya kifaa kinachoitwa kioo, ambacho kinatuonyesha sura zetu
zilivyo. Wengi wanapenda kutumia muda mwingi ndani ya sehemu ya nyumba palipo
na kioo kwa maana ya kuwa sehemu ya kuvalia yenye kioo. Hapo mahali ni kwenye dressing table! Meza ya kuvalia kwa lugha
nyingine dressing table ikiwa
imeambatanishwa na droo, kioo na kiti ni fenicha muhimu mno ndani ya nyumba ya
kuishi.
Kuna aina kadha wa kadha za
fenicha ambazo ni kama zimepuuzwa katika baadhi ya nyumba. Meza ya kuvalia ni
le aina ya fenicha ambayo ni muhimu sana kuwa katika kila nyumba ambapo sio tu
kwamba inaongeza uzuri na rehema ndani ya nyumba bali pia inaonyesha
ushirikiano mkubwa katika matumizi yake.
Vioo vilivyoko kwenye meza
ya kuvalia vinasaidia mno kwa kuwezesha wewe mwanamke mzuri na mwanaume bomba
kujiandaa vyema wakati wa kuvaa na hivyo kutoka nyumbani ukiwa unajiamini. Kiti
kidogo ama kistuli cha meza ya kuvalia kinakusaidia kukaa na kujiandaa kwa
kuvaa, kutupia na kuweka vipodozi vyako bila wasiwasi huku ukijitazama kwenye
vioo. Hasa wanawake huwa tunachukua muda wa kujiandaa na kupaka vipodozi, kiti
kinahtajika sana wakati huo. Pia fahamu kuwa hiki kiti au kistuli cha meza ya
kuvalia huwa ni kidogo kwa hivyo hakisababishi mrundikano kwenye chumba chako.
Droo za meza ya kuvalia hutumika kuhifadhi vitu mbalimbali hivyo kuwa rahisi kupata kile unachohitaji mara moja.
Droo za meza ya kuvalia hutumika kuhifadhi vitu mbalimbali hivyo kuwa rahisi kupata kile unachohitaji mara moja.
Kwa kawaida huwa meza ya kuvalia ina droo 3
hadi 4 ambazo hutumika kuhifadhia vitu kadhaa. Meza hii inaakisi utambulisho wa
mtu anayeitumia. Kwa mfano, bachela atajaza meza yake kwa kila aina ya
deodoranti, pafyumu, nguo za ndani, mikanda na wakati mwingine hata mipira ya
kiume miwili au mitatu! Mwanamke naye anaweza kuhifadhi vitu kama vile nguo
(kwenye droo zake), kuhifadhi vipodozi na manukato, kuhifadhi vitupio kama
bangili, shanga, mikufu na hereni. Meza hii pia huwa hutumika kuhifadhi vitu
vya faragha kama nguo za ndani kwa vile mara nyingi huwa inawekwa chumba cha
kulala.
Meza za kuvalia zinapataikaan za aina na mitindo mbalimbali. Zipo za mbao, chuma na hata plastiki ngumu na kadhalika. Unaweza kununua yeyote ambayo inafaa kwa nyumba yako na inaendana vyema na mapambo yako mengine ya ndani. Gharama pia zitatofautiana kuendana na kifaa kilichotumika kutengenezea meza na pia aina ya kioo, anasema seremala Musa Hussein. Meza nyingine huwa zina vioo viwili ambapo unaweza kujiona nyuma na mbele.
Meza za kuvalia zinapataikaan za aina na mitindo mbalimbali. Zipo za mbao, chuma na hata plastiki ngumu na kadhalika. Unaweza kununua yeyote ambayo inafaa kwa nyumba yako na inaendana vyema na mapambo yako mengine ya ndani. Gharama pia zitatofautiana kuendana na kifaa kilichotumika kutengenezea meza na pia aina ya kioo, anasema seremala Musa Hussein. Meza nyingine huwa zina vioo viwili ambapo unaweza kujiona nyuma na mbele.
Unaweza kununua meza iliyotengenezwa tayari au
unaweza kupeleka oda yako kwa fundi akakutengenezea. Kama fundi atafanya kazi
nzuri meza ya kuvalia ya kubuni mwenyewe inaweza kukupa burudiko la kudumu. Kufahamu
mitindo iliyopo tembelea mitandao na soma majarida mbalimbali yanayohusu
mapambo ya nyumbani. Wakati wa kuoda au kununua ni vyema kuzingatia sehemu au
chumba utakachoweka seti yako hiyo. Kila mmoja ana ladha yake binafsi
linapokuja swala la kununua fenicha za nyumbani, ila ni vyema kupokea ushauri
wa wanafamilia wengine ama hata wabunifu wa ndani kabla ya kuamua kununua aina
fulani ya meza ya kuvalia.
Kwa kawaida meza hii inakaa chumba cha kulala
ingawa baadhi ya wabunifu wa fenicha wanashauri iwekwe bafuni kama una eneo kubwa,
na hata zipo meza za kisasa zaidi zilizounganishiwa umeme kwa ajili ya kutumia
vikaushia vywele na visafisha uso vya mvuke.
Meza ya kuvalia ilivumbuliwa kukusaidia
kujiandaa ukiwa huru na amani tele kwenye chumba chako mwenyewe cha kulala.
Unaweza kujiremba na kujipendezesha kwa raha zako kwenye meza hii.
Unaweza sasa ukatafakari ni
kwa jinsi gani unaweza kuwa mbunifu kwa kutumia dressing table na droo zake maridadi bila kusahau kioo na kiti chake
cha staili. Ni fenicha muhimu mno kuwa nayo. Pia usisahau kuwa meza ya kuvalia
ni kituo cha vitu vyako vingi ambavyo vingeweza kuwa vimewekwa maeneo mengine
chumbani na kuleta muonekano wa mrundikano. Chumba cha kulala kinasemekana hakijakamilika bila kuwa na eneo
hili la kuvalia kwenye ukuta wake mmojawapo.
Makala hii imeandaliwa na Vivi Machange ambaye ana mapenzi makubwa juu ya muonekano wa makazi. Kwa maoni au maswali tuma kwenda 0755 200023 au viviobed@yahoo.co.uk
Makala hii imeandaliwa na Vivi Machange ambaye ana mapenzi makubwa juu ya muonekano wa makazi. Kwa maoni au maswali tuma kwenda 0755 200023 au viviobed@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment