Monday, June 20, 2016

Unajiuliza uweke TV yako juu ya kabati lake au uipachike ukutani? Jibu hili hapa..



Fahamu faida na changamoto za maeneo mawili ya kuweka luninga

Uko kwenye mchakato wa kuweka luninga na unafikiria uiweke juu ya kabati la luninga au uisimike ukutani? Kuna mengi ya kujua kwenye kuchagua haya maeneo mawili kabla hujafanya uamuzi wa mwisho.

Unapoamua kama
uitazame luninga yako kupitia ukutani au kwenye kabati kuna mambo kadhaa ya kuzingatia. Kuangalia faida na changamoto nitakujuza ukweli unachopaswa kufahamu ambapo utapata jibu la njia utakayochagua ili iwe sawa kwa mtindo wako wa maisha na unadhifu wa nyumba vilevile.

Tangu kuingia kwa matoleo ya luninga flati, kuzisimika ukutani imekuwa ni njia mbayo inafanya zionekane na kutizamika vizuri zaidi. Vilevile kusimika ukutani siku hizi imekuwa hata maarufu zaidi kwa sababu huhitaji kuweka chochote sakafuni kwa ajili ya kuishikilia. Namna hii inakifanya chumba ambacho luninga imewekwa ukutani kuonekana kuwa na nafasi kubwa. Pia ni njia salama kwa watoto wanaopenda kuchezea waya au kupanda juu ya kabati na pengine kuidondosha na kuivunja luninga yako ya gharama. Zaidi ya muonekano wa kiwango na mvuto, njia ya kusimika luninga ukutani ni sahihi hasa kwa wale wenye nyumba ndogo.

Faida nyingine ya kuwa na luninga ukutani ni kwamba unaweza kutumia spika ndogondogo za kuweka darini kwenye kona za chumba. Hii ina faida sana kwani waya zote zinajificha hakuna inayoonekana wazi.

Tukija kwa upande wa njia ya kuweka luninga juu ya kabati ni kuwa inachukua nafasi kubwa kuliko ile ya kusimika ukutani.  Makabati ya kuwekea luninga yanakuja kwa rangi nyeupe, nyeusi na hata katika finishing mbalimbali za mbao na chuma. Ni ukweli kuwa makabati ya luninga yanachukua nafasi kubwa ya sakafu na chumba. Kwa miundo yake mengi yameongezewa maeneo ya hifadhi kama vile droo na shelfu ambapo kwa upande mwingine ni faida kwamba unaweza kuhifadhia humo muvi, vitabu na hata michezo ya kwenye luninga na hii inakusaidia kuweka mpangilio wa mahali luninga ilipo.

Ni vyema upate majibu ya maswali haya matatu wakati wa kuchagua njia sahihi kati ya hizi mbili ya kwamba usimike luninga ukutani au uiweke juu ya kabati.

·        Chumba unachotaka kuweka luninga kina ukubwa kiasi gani?
·        Ni kiasi gani cha hifadhi kinahitajika kwa ajili ya muvi na michezo ya video?
·        Je, kuna hatari yoyote ya kusababisha luninga ianguke  na kuvunjika?

Jambo la muhimu ni kuwa, kwa njia yoyote utakayochagua, usalama iwe jambo la kuzingatia zaidi. Baada ya hapo, hifadhi nayo ni muhimu. Na pia usisahau muonekano, ambapo unachangia kukupa msukumo wa kuchagua kabati la luninga au ukutani. Kila mmoja anataka ndani ya nyumba yake kuonekane kusafi na kuwa na mpangilio ili kuvutie.

Kwa hii elimu ndogo, yeyote anaweza kuamua atizame luninga yake ikiwa  kabatini au ukutani.


Simu 0755 200023

No comments:

Post a Comment