Ulishafikwa
na tatizo la kuingia nyumbani na mara kichwa kinaanza kukuuma kwa hewa nzito
iliyopo? Au labda umegundua harufu ambayo huifurahii ndani ya nyumba yako na
haielekei kuisha? Hizi zote ni dalili za haja ya kuboresha hali ya hewa ya
ndani ya nyumba.
Watoto
na watu wenye mzio wanaweza kuhisi mabadiliko ya hewa ndani ya
nyumba hata yawe
madogo kiasi gani. Ila pia matokeo ya hewa nzito ndani ya nyumba yanaweza
kuwasababishia wanafamilia matatizo ya kiafya miaka mingi ijayo endapo tatizo
hilo halitafutiwi suluhisho mapema.
Inawezekana
mwanzoni likaonekana ni jambo gumu la kufanya, ila cha kushangaza ni kuwa
kuboresha hali ya hewa ya ndani ni rahisi sana. Unachotakiwa ni kuzingatia tu
mambo machache, na unaweza kuwa na nyumba huru na harufu na isiyokuwa na
vichafua hali ya hewa.
Uboreshaji
wa uingizaji njia za kuingiza hewa ndani ni namna kuu ya kuongeza ubora wa hewa ya ndani. Wakati
hewa inapoanza kuwa nzito na hakuna uingizaji wa iliyo safi hapo ndipo na
vichafua hewa ndani ya nyumba vinapoanza kujijenga. Na changamoto kubwa ya
nyumba zetu za kisasa ni kuwa zimezibwa kila mahali na ni kawaida kukuta
milango na madirisha yamefungwa kwa muda mrefu kuliko yanavyofunguliwa. Njia
rahisi ya kuondoa tatizo hili ni kufungua madirisha kila siku na pia kuwasha
feni.
Jambo
lingine ni kuzingatia usafi wa jumla, kwamba sakafu ziwe safi na zisafishwe kila inapobidi. Kwa kuruhusu
taka, nguo chafu, vumbi na uchafu mwingine kujijenga unakaribisha uwezekano wa kuharibu
hali ya hewa ndani ya nyumba. Usiruhusu vyombo vichafu vijazane kwa muda mrefu
bila kusafishwa, na pia usihifadhi nguo chafu zinazonuka majasho kwa muda mrefu
bila kufuliwa. Futa vumbi kila wakati.
Kama
una vifaa vya kisasa vihusianavyo na maboresho ya hewa ya ndani kama vile
viyoyozi hakikisha kuwa vinafanyiwa usafi wa mara kwa mara ili chujio zake
zisibebe vumbi na kushiriki kulisambaza. Pia feni zisafishwe. Bila kusahau
kutumia marashi za kupuliza ndani ya nyumba pale inapobidi.
Epuka
vichafuzi vya hewa ya ndani kama kweli umepania kuboresha hali ya hewa ndani ya
nyumba yako. Kitu cha kwanza cha kufanya ni kuepuka kinachoharibu hali hiyo ya
hewa. Kwa mfano kuna fenicha na gundi
zinazotoa harufu kipindi chote, madawa, manukato yatumikayo kwenye dawa za
kusafishia. Na pia kuna harufu zinaingizwa ndani ya nyumba kupitia fenicha
mpya, magodoro, mazulia au hata rangi ya ukutani.
Uvutaji
wa sigara ndani upigwe marufuku kabisa kwani ndio kichafuzi namba moja cha
hewa. Inaweza kuwa maumivu kama mvutaji ni mwenye nyumba lakini hakuna jinsi
itabidi iwe hivyo.
No comments:
Post a Comment