Kwa
miaka kadhaa sasa baadhi ya Watanzania wamekuwa na utamaduni wa kupamba nyumba
zao kwa kutumia miti bandia ya krismasi kipindi cha msimu wa sikukuu hiyo. Miti
hii imepata umaarufu kwa kasi kwani inasaidia kupunguza usumbufu na pia unaweza
kuhifadhi baada ya sikukuu na kutumia tena mwaka inayofuata.
Kutokana
na kuwepo kwa
miti mbalimbali ya bandia ya krismasi inayouzwa, inaweza kukuwia
changamoto kupata ulio sahihi. Kwa kuzingatia yafuatayo itakurahisishia
mchakato huo.
Kwanza
kabisa fahamu ukubwa wa mti unaohitaji. Na hii itakusaidia pale ambapo unajua
kabisa kuwa ni wapi unauweka iwe ni kwenye ujia, kona ya chumba au katikati. Ndipo
unafahamu ni eneo kiasi gani unalohitaji kufunika. Unafahamu upana na urefu, usinunue
mti mrefu kiasi kwamba utagusana na dari.
Nunua
mti wenye ubora wa juu. Moja ya faida ya mti wa krismasi wa bandia ni kwamba ni
uwekezaji wa miaka mingi. Kufahamu kiwango cha ubora angalia majani yake. Mti
wenye majani yaliyofunga hata kuficha shina ni bora kuliko ule ulio wazi.
Halafu pia miti ya bandia ya krismasi yenye ubora wa hali ya juu huwa ina
stendi za chuma. Kama lengo lako ni mti bora, epuka ile yenye stendi za
plastiki.
Stendi
imara inakuhakikishia mti kutoinama au kutojikunja upande mmoja, hata pale
mapambo inayobeba yanapokuwa ni mazito. Baadhi ya miti ambayo ubora ni wa hali
ya juu zaidi, stendi zake za chuma zinakuwa zimeongezewa mipira ili kulinda
sakafu.
Ingawa
miti ya bandia ya krismasi inaweza kuwa na mchanganyiko wa maumbo mawili ya
majani yake, haijalishi ni upi utanunua ila cha kuzingatia ni kununua ambao ngalao
wenye muonekano wa mti hai. Kwa mfano ipo miti ambayo rangi zinapishana
kuendana na eneo la mti kama ni shina, majani yaliyokomaa na yale machanga. Kwa
mfano tawi au shina linaweza kuwa na kijani kinachoelekea kwenye rangi ya
udongo wakati majani yaliyokomaa yakiwa na kijani kizito huku yale mabichi
yakiwa na kijani mpauko. Hii yote ni kujaribu kuongopea jicho kwamba mti ni
hai.
Nunua
mti ambao utakubaliana na ulivyopanga kuupamba. Hakikisha matawi ni imara
kuweza kubeba mapambo unayotaka kuuwekea.
Fahamu rangi unayotaka kabla hujanunua. Waliokulia kwenye nyumba ambazo zina kawaida ya kupamba kwa mti wa krismasi wanajikuta wakidhani kwamba mti wa krismasi sahihi ni ule wanaoufahanmu toka utotoni. Mingi ya miti hiyo ya zamani ilikuwa rangi ya kijani tu, ila kwa miaka ya sasa tumeona miti ikija kwa rangi nyeupe, silva kama barafu na kadhalika. Usifungwe na fikra za kuwa mti wa krismasi lazima uwe wa kijani. Nunua mti ambao utakutengeneza kumbukumbu nzuri na muhimu kwako na familia yako.
No comments:
Post a Comment