Badala
ya mtindo wa zamani wa kuwa na redio, siku hizi mambo ni kwa home theatre.
Nimeongea na Bi Jacky Ngoma 0679 414 133 ambaye ni mtaalam wa mambo haya kutoka kampuni ya Jaden Home Store walioko
Kijitonyama Dar es Salaam, na hapa anatuelimisha zaidi home there ni kitu gani
haswa. Anaanza kwa kusema kuwa Home theatre ni
mfumo wa muziki na luninga ambao
unawekwa nyumbani kwa lengo la kuangalia muvi
kwa jinsi ile ile ya kama vile unavyokua kwenye ukumbi wa sinema.
Mfumo
huu unakuwezesha kuona picha zenye ungavu wa hali ya juu na sauti nzuri ili
kuzipa uhai filamu zako upendazo ila ni vitu kadhaa vinavyoweza kufanikisha
hilo. Vitu hivyo ni luninga, deki ya DVD na spika. Kitu pekee kinachomfanya
mtazama muvi akiwa kwenye ukumbi wa sinema kubakiwa na kumbukumbu ni ile sauti
ya pale.
Spika
za home theatre zinakuja kwa maumbo na ukubwa mbalimbali, kuanzia kubwa ndefu
za kusimamisha zenyewe hadi za kuweka kwenye shelfu hadi nyembamba ambazo
zinawekwa ukutani. Ni rahisi tu kwasasa kukutana na spika ndogo kimuonekano
lakini zenye kufanya kazi vizuri sana za makampuni kama Sony LG, Samsung na
kadhalika.
Ingawa
home theatre inafaa hata kwenye sebule za kawaida, ila kama una chumba ambacho
kimetengwa maalum kwa kazi hii, unakuwa na uhuru zaidi wa kuchagua spika zile haswa
unazotaka. Bila kujali ukubwa au mpangilio wa chumba na kuweza kuziweka maeneo
sahihi ili kuleta matokeo mazuri. Vinginevyo kama unajaribu kuongeza mfumo huu kwenye
chumba ambacho tayari kipo na matumizi mengine, pengine hutakuwa na wigo mpana
wa kuchagua spika za kusimama huru ambazo ungetaka. Huenda wewe au mwenzio wa
muhimu asipende sebule iwe na msongamano kutokana na ukubwa wa spika. Kama ni
hivyo basi spika za kupachikwa ukutani au darini inawezekana kuwa ndio
zitakufaa. Kwa wale ambao wamebahatika kuwa na chumba maalum uchaguzi wowote
kwao inawezekana.
Mpangilio
na muonekano unaguswa na uwepo wa home theatre kwahivyo unapotaka kununua
chagua kwa makini.
Vilevile
kama tujuavyo unaponunua vifaa vya umeme ni muhimu pia kuwa na uhakika kuwa
vifaa hivyo vina uwezo wa kutumika pamoja na vingine ulivyonavyo nyumbani.
Unatakiwa kufahamu kuwa kifaa kina maeneo ya kutosha ya kuunganishwa na kingine
kwa maana kama tulivyosema huu ni mfumo kwahivyo ni vifaa kadhaaa
vinaunganishwa pamoja ili kuleta matokeo fulani.
Mara unapokuwa umekamilisha mfumo wa vifaa vyote unavyohitaji kwa ajili ya home theatre kilichobakia ni kupata rimoti moja ya kuviendesha vyote kwa pamoja, labda uwe ni mtu unayependa kutumia rimoti tano ili uweze kuangalia filamu moja! Inapaswa kuchagua na kuprogramu rimoti moja ili kufanya maisha ya mtazamaji wa kila siku nyumbani yawe rahisi.
Karibu
kwenye ulimwengu wa home theatre ili uweze kufurahia sauti na picha za kiwango
cha hali ya juu zaidi kutoka kwenye vifaa vyako vya burudani uwapo nyumbani.
Kwa wewe unayehitaji Home Theatre ukiwasilaiana na Jacky mwambie umeona tangazo kwa Vivi
No comments:
Post a Comment