Msimu
wa sikukuu unakaribia na wapo wanaopenda kuwa na wageni wa kulala nyumbani
kipindi hicho. Ila hawapendi kupoteza mpangilio na usafi wa nyumba kutokana na ugeni.
Tuangalie
unachotakiwa kufanya ili kudumisha usafi na mpangilio kwenye maeneo ambayo
wageni wa kulala wanaingia wawapo nyumbani kwako. Maeneo hayo ni
nje ya nyumba,
varanda, sebuleni, chumba chao cha kulala, bafuni na jikoni.
Nje
ya nyumba na varanda
Ili
kuepuka uchafu kuingizwa ndani kupitia viatu, hakikisha maeneo ya nje ya nyumba
ni safi.
Weka
tandiko la mlangoni eneo la varanda kwa nje na ndani ili wageni waweze kufuta
viatu kupitia tandiko la nje na nyayo kupitia la ndani.
Weka
kitundikio cha makoti, skafu na kanga varandani ili wageni wanapoingia ndani waweze
kutundika nguo hizi endapo zitakuwa zimebeba uchafu wowote toka nje walikokua.
Baadaye aidha zitavaliwa tena au kufuliwa.
Kwenye
chumba cha kulala wageni
Fanya
utandikaji uwe rahisi kwa kuweka duveti (linasaidia kupendezesha, kutandika
haraka na kwa urahisi) na mito michache angalau miwili tu. Kuweka mito nane ni
kujiongezea kazi kwako au kwa wageni.
Ondoa
mrundikano kwenye maeneo yote ya chumba hiki ili wageni waweze kutumia meza iwe
ni ile ya kuvalia au nyingine kwa ajili ya kuwekea vitu vyao. Chumba kisichokuwa
na mrundikano ni rahisi kusafisha. Kama
inawezekana chumba kiwe na kabati la nguo au stendi pamoja na vitundikio vya
nguo.
Chumba
kiwe na kindoo cha taka na tenga la kuwekea nguo chafu.
Kwenye
bafu la wageni
Mara
moja kila siku nguo chafu ziondolewe zikafunliwe.
Matumizi
ya sabuni ya maji badala ya ya kipande ni mazuri zaidi kwa bafu la wageni kiafya
na pia haichafui kama ya kipande.
Wote
tunajua ambavyo hatupendi tunapofua kukutana na taulo lililofutiwa vipodozi.
Suluhisho la tatizo hili kwenye bafu la wageni ni kuweka kitambaa au tishu
ambazo zitafanya kazi hiyo na ukatoa maelezo kwa wageni wako kuhusu kitambaa
hiki. Unaweza kukitupa mara wageni wakiondoka.
Lazima
kuwa na vihifadhio vya taulo ili kuepuka kuzikuta chini hapo baadaye.
Sebuleni
Toa
maelekezo ya namna ya kuwasha vyombo vya burudani na matumizi ya rimoti. Hii
itakuepusha kuja kuviseti upya endapo vitavurugwa.
Jikoni
Waonyeshe
wageni vinywaji vinakohifadhiwa ili waweze kujiandalia wenyewe. Waonyeshe kila
kitu endapo watahitaji kunywa chai, kahawa, kakao, vinywaji laini na vyoyote
vile vingine.
Weka
matunda na vitafunwa kama biskuti, korosho na karanga mahali pa wazi ili wageni
waburudike wakati usio wa chakula. Hutakuwa na wasiwasi kwamba chakula
kimechelewa na wageni wana njaa
Mwishoni
kama wageni wanataka kuingia jikoni wasaidie, waruhusu! Hakikisha tu kwamba kazi
wanazosaidia ni nyepesi.
No comments:
Post a Comment