Monday, May 1, 2017

Uzoefu wangu wa safari ya kutembelea Saadani National Park


Habarini wapenzi,

Bila shaka wapo wengi wanaotaka kutembelea vivutio nchini mwetu lakini hawajui waanzie wapi au japo hawapati mwongozo kutoka kwa waliokwisha tembelea maeneo hayo.

Hivyo basi nimeamua kuwashirikisha japo kwa uchache juu ya safari yangu ya siku 3 kutembelea hifadhi ya Taifa ya Saadani.

Kutokana na uwepo wa sikukuu ya mei mosi ambayo ingefanya mapumzikoni ya mwisho wa wiki kuwa marefu, kama kawaida yangu nilifikiria kitu cha kufanya wakati wa mapumziko hayo.

Nikaamua nataka kwenda na kuona ambapo sijawahi kwenda. Kwanza kabisa nilitafuta watu ambao wana organise safari kama hizi. Nilipowapata nikafanikiwa kununua tiketi ambayo ilijumuisha usafiri, malazi, chakula na kiingilio cha mbugani. Nikawa mmoja wa wateja na huku kukiwa pia na wateja wengine ambao wote tulisafiri pamoja. Kumbuka kuwa unaposafiri kwenye kundi ni gharama nafuu kuliko kusafiri mmoja mmoja.

Safari ilianzia Dar, Afrika Sana ambapo waandaaji walifanya kazi nzuri na mipangilio mizuri na tukaanza safari saa kumi juu ya alama. 
Kuna njia mbili za kuweza kufika Saadani, ya Bagamoyo na ya Wami. Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha njia ya Bagamoyo haikufaa hivyo tukapita ya Wami.

Kutoka barabara kuu ile ya lami pale Wami hadi Saadani kwa mwendo wa kasi ni masaa mawili.

Kwenye saa mbili kasoro tukaingia Saadani. Tukakaribishwa vyema kwa chakula cha usiku na malazi. Malazi yanaweza kuwa kwenye lodge, rest house au tents kuendana na hela yako/waandaaji.
Endapo utataka kwenda huna haja ya kubeba shuka kwani taulo na malazi yapo, kwa bafuni utatakiwa kubeba mswaki na dawa ya meno, chanuo na vipodozi vyako tu. Pia wakati wa dinner na tukapewa muongozo kesho yake. 

Tukaambiwa kuwa kwa vile kipindi hiki ni cha mvua (kwa profession yao wanaita low season) wanyama wana kawaida ya kujificha kwahivyo by saa moja asubuh tunatakiwa tuwe tumeshaingia porini ndipo turudi kwenye saa nne kwa ajili ya kifungua kinywa. Hii ya mapema hivi ni ili kuwahi wanyama kabla hawajajificha.

Tukaenda porini tukafanikiwa kuwaona baadhi ya wanyama kama vile twiga, nguruwe pori, ndege mbalimbali na nyumbu. Baada ya hapo tukarejea restaurant ambapo ilikuwa ni wakati wa chai na baada ya chai tukaanza utalii wa beach.
Tafadhali fahamu kuwa hii ni mbuga pekee Afrika ambayo inaunganika na bahari. Kama ni mpenzi wa kuogelea utakapoitembelea kumbuka kubeba swimming costume.
Hakika niliifurahia sana beach kwa michezo mbalimbali pamoja na wenzangu, kuogelea pamoja na kwamba mvua zilikuwa zinaendelea kunyesha.

Baada ya dinner na some drinks na socializing tukaenda kujipumzisha hadi kesho yake ambapo tuliamkia supu ya mbuzi na capati. Kwa misosi waandaaji nisiwe na hiyana walijiaanda vyema sana. Baada ya supu hii na chai tukarudi vyumbani kwenda kupaki kwa ajili ya safari ya kurudi.

Kwenye saa sita mchana tukaanza safari ya kurejea Dar na hapo ukawa ndio mwisho wa safari yangu.

Ndio hivyo wapenzi! Ukiwa na swali kuhusu safari hii au unataka kununua kati ya viwalo kama nilivyovaa unaweza nicheki kwenye 0755 200023. Asante kwa kusoma!

No comments:

Post a Comment