Wednesday, November 30, 2016

CHANZO CHA GHARAMA KUBWA ZA UPIMAJI ARDHI NA SULUHISHO LAKE.

Na Surveyor James aloyce
-Kumekua na malalamiko makubwa sana toka kwa wananchi juu ya gharama kubwa za malipo kwenye upimaji ardhi.

Leo ningependa mfahamu nini chanzo cha gharama hizo 

1. Zoezi la upimaji linashirikisha viongozi wengi katika serikali wa ngazi mbalimbali  huku kila mmoja akiwa na umuhimu wake na lengo likiwa ni
kuzuia migogoro ya ardhi mfano mwenyekiti na mtendaji wa kijiji(kijijini), afisa ardhi,mipango miji, mpimaji(manispaa/halmashauri), mpimaji wa mkoa(mkoani), mpimaji msajiliwa, mkurugenzi wa upimaji ardhi.

2. Elimu kuhusu mambo ya ardhi, jamii kwa ujumla ina uelewa mdogo sana kuhusiana na maswala ya ardhi ivyo kupelekea gharama pindi unapotaka pima eneo lako, mfano  (kununua ardhi bila kujua ipo kwa ajili ya matumizi gani n.k)

Suluhisho ya gharama kubwa za upimaji;

1.Upimaji shirikishi, Ni moja ya njia sahihi kabisa ya kupunguza gharama za upimaji,  kwenye upimaji ukiwa mtu mmoja na kiwanja chako kimoja au viwili ni lazima gharama zitakua kubwa kutokana na kulipia gharama zote za uendeshaji zoezi hilo kwa mtu mmoja, mfano (gharama za usafiri, mashine za upimaji, wafanyakazi wa ziada na ufuatiliaji wa zoezi la upimaji) ivyo vyote vitagharamikiwa na mtu mmoja. Ila mkiwa wengi ina maana hizo gharama mtachangia watu wengi ivyo kufanya gharama ziwe ndogo.

2. Elimu kuhusu mambo ya ardhi, Kila raia ajitahidi kupata elimu ya ardhi kabla ya kumiliki kipande chochote cha ardhi kwa kutuona wataalam.
Kwa upande wangu nimekua msaada sana kwenye hilo. Ivyo kaa karibu, pia unaweza kunialika katika jamii yako kuwaelemisha na page zangu za mitandaoni, karibu ofisini kwangu pia na pia kuwa huru kunipigia kwa namba zangu za simu muda wowote.

Facebook; Surveyor James Aloyce
Instagram; Surveyor Aloyce
Contact; 
WhattsApp;0713778937
            Call;0754619189
            Call;0785779111
By Surveyor James Aloyce

Gold Land company Ltd

No comments:

Post a Comment