Linapokuja
swala la kufanya chumba kidogo ndani ya nyumba kionekane kikubwa au hata ndani
ya nyumba ndogo kuonekane ni kukubwa na kumfanya aliyemo kupata hisia ya nafasi
zaidi, kuna kanuni kuu mbili muhimu unazotakiwa kuwa nazo kichwani. Kanuni hizo
ni kwanza kuruhusu
mwanga kwa kadri iwezekavyo na pili ni kutumia vihifadhio
vya aina mbalimbali.
Makala
hii itakujuza namna unavyoweza kutumi kanuni hizi mbili kutengeneza chumba
chenye nafasi na mpangilio.
Kanuni
ya kwanza na muhimu ni mwanga. Mwanga unavyokuwa mwingi chumbani, ndivyo
unavyopata hisia za kuwa na nafasi kubwa
na wepesi uwapo chumbani. Vilevile chumba kinapokuwa cha mwanga hafifu,
ndivyo kinavyozidi kuonekana kidogo na unahisi kuelemewa fulani uwapo ndani.
Sasa
basi, kwakuwa unataka chumba chako kiwe na mwanga kadri iwezekanavyo, ni vyema
kutumia rangi nyepesi ukutani na mandhari nzima ya chumba kwa ujumla. Rangi
sahihi kwa dari na kuta ni nyeupe na krimu. Ni vyema kufahamu kuwa pamoja na
maeneo haya kuwa meupe bado unatakiwa kuwa na fenicha za rangi nyepesi kwenye
chumba kizima ili kupata mwanga unaoutaka na utakaowezesha kufanya chumba
kionekane kikubwa.
Madirisha
makubwa ni njia nzuri ya kuruhusu mwanga wa jua kuingia ndani kwa wingi. Ni
njia rafiki kwa mazingira na pia gharama nafuu kwani huhitaji kuwasha nishati
kwa ajili ya mwanga mchana.
Endapo
huna madirisha ya kutosha au yaliyopo ni madogo sana, ndipo inakulazimu
kuutafuta mwanga kwa njia nyingine kama vile kutumia balbu na vioo. Vioo
vikubwa vilivyowekwa kutazamana na dirisha vinasaidia kuakisi mwanga kutoka nje
na kuurudisha ndani. Vilevile milango yenye panel za vioo inafanya vyema zaidi
kuingiza mwanga ukilinganisha na ile iliyozibwa kotekote. Pia maeneo
yanayong’aa iwe ni makabati au sakafu yanasaidia kuongeza mwanga ndani na hivyo
kufanya chumba kionekane kikubwa.
Kanuni
ya pili ya kufanya chumba kidogo kionekane kikubwa ni kuwa na vihifadhio vingi
aina mbalimbali kadri iwezekanavyo. Kwa mfano, mashelfu ya ukutani ni njia
nzuri sana ya kuweka mpangilio katika chumba chochote Yanaweza kuwa ni mashelfu
ya wazi kama ya vitabu au ni yaliyo ndani ya makabati. Uzuri wa shelfu za
ukutani ni kwamba unaweza kuziweka kwenye ukuta wa juu ambao usingetumika kwa
kazi nyingine.
Mashelfu
unaweza kuyatumia kuhifadhi chochote kutokana na chumba yalipo. Yatumie
kuhifadhi vibakuli, sahani, viatu, nguo za kukunja, vitabu, michezo na midoli
ya watoto na vitu vingine vingi.
Vivi anakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Endapo unahitaji ushauri wowote uwe ni kununua fenicha au kuchagua rangi au chochote kuhusu kupendezesha nyumba yako tafadhali tuwasiliane....Simu 0755 200023
No comments:
Post a Comment