Muonekano
wa nyumba kwa sehemu kubwa unachukuliwa na rangi na ndipo naweza kujiamini kwa
kusema nyumba ni rangi. Karim Msheki
ambaye ni mtaalam wa kuchanganya rangi anatueleza maana na namna ya
kuchagua rangi tunapotaka kupendezesha nyumba zetu.
Anasema,
kuna mafungu makuu mawili ya rangi ambayo ni rangi za msingi na zile za
sekondari. Kila fungu lina rangi 3 ambapo za msingi ni njano, nyekundu na bluu.
Na za sekondari ni kijani, chungwa na zambarau. Hizi za sekondari ni mchanganyiko
wa hizi 3 za msingi.
Rangi
ni somo la kina kimtizamo wa sayansi, hisia, muonekano na dini, ila huhitaji
kuwa daktari wa filosofia ya rangi bali kuelewa yale mambo machache ya muhimu
kwako.
Kwanza
kabisa, rangi zina chanzo chake ambacho ni mwanga wa jua. Kwahivyo rangi ni
jinsi unavyoimulika! Ndio maana pasipo mwanga huoni rangi yoyote.
Rangi
inaweza kuelezewa katika nyanja 3 ambazo ni jina la rangi, kivuli cha rangi na
akisi ya rangi.
Njano
inaonekeana kama jua, na inaelezea ubora ambao jua linautoa. Njano chumbani
inaleta maana hiyohiyo kama ya jua.
Nyekundu
inazungumzia moto na damu. Inaambatana na uchangamfu, nia na kukomalia jambo.
Ni vyema kujua kuwa kwa tabia hizi chumba kilichopakwa rangi nyekundu kinaleta
kisia ya kuwa ni kidogo kimuonekano.
Bluu
ni kinyume cha nyekundu. Inaelezea hisia za utulivu na umbali. Umbali
unasababisha chumba kionekane kikubwa.
Kijani
ni muunganiko wa njano na bluu na hivyo ina tabia ya rangi zote mbili. Hakuna
sehemu inayoweza kuwa tulivu na ya kustarehe kama kukaa kwenye viti vilivyowekwa juu ya ukoka
wa kijani kibichi chini ya kivuli cha kijani cha miti katikati ya siku ya joto
kali.
Kivuli ni
Nyanja nyingine ya kuelezea rangi. Ni ile hali ya wepesi au uzito wa rangi
kutoka kwenye jamii ya rangi hiyo. Kwa mfano kijivu nyepesi inakaribia nyeupe
wakati ile nzito ikikaribia kabisa nyeusi, pinki ni kivuli cha jamii ya
nyekundu na vivyo hivyo kwa damu ya mzee.
Cha maana
zaidi ni kufahamu hili swala la kuchagua rangi kwa ajili ya kuta na pia vitu
vilivyomo ndani ya nyumba. Kanuni hizi mbili zitakujibia jambo hili:
1. Kwa lengo ya kupendezesha ni
kwamba background zinatakiwa kuwa na rangi nyepesi kuliko vitu. Huenda
unajiuliza maana yake ni nini, ni kwamba kuta, dari na sakafu zinatakiwa ziwe
na rangi nyepesi wakati fenicha na sanaa za ukutani zikiwa na rangi nzito.
2. Kitu (hapa si yale maeneo makubwa
ya background) kinapokuwa kikubwa ndivyo
kinavyotakiwa kiwe kwenye kivuli cha upande ule wa rangi ambao ni nyepesi na
kinyume chake ni kwamba kinapokuwa kidogo uzito wa rangi unatakiwa uongezeke. Hii
ni katika kusadia hivyo vitu vidogo navyo vichomoze vionekane. Kutokana na
kanuni hii ni kwamba vile vitu vikubwa kama zulia kwa mfano vinapaswa kuwa vya
rangi nyepesi kuliko vile vidogodogo kama mito ya kwenye makochi na vivuli vya
taa za mezani.
Kwa elimu
hii ndogo ya rangi ni imani kuwa utachagua rangi ya kuta na vitu kwa uelewa.
Simu 0755 200023
No comments:
Post a Comment