Kwa
nyumba za kisasa za nyakati hizi, wenye nyumba wengi wanapenda kutumia mabafu
ya cubic. Haya ni mabafu ambayo ni kichumba kidogo cha kuogea ambacho
kinasimikwa ndani ya chumba cha bafu. Mengi ya mabafu haya ni ya kioo na mara
yanaposimikwa yanaweza kudumu maisha yakie
ndelea kutumika bila tatizo. Yanapendwa
kwenye nyumba nyingi zenye watu wadogo na wa makamo na hata wazee.
Zifuatazo
ni faida zake:
Yanarahisisha
usafi na utunzaji wa bafuni
Mara
unapokuwa umesimika bafu lako la cubic kinachotakiwa ni kutumia na kusafisha ndani
mwake ambapo ni eneo dogo sana badala ya
chumba kizima cha bafu. Hii imerahishiwa kwa ajili ndipo hapo tu panapogusana
na maji wakati wa kuoga. Kwahivyo kazi ya kusafisha na kuweka bafu kavu ni
ndogo ulishangisha na mabafu yasiyokuwa
na cubic hizi. Hii inamhakikishia mtumiaji wa bafu afya njema na usafi siku zote.
Yanachukua eneo dogo
Mabafu ya
cubic ni madogo na kiukweli yanafiti karibia katika kila bafu. Unachohitaji tu
ni kuta za kona kwa ajili ya kulisimika. Kwa makazi ya kisasa ya nyumba ndogondogo
hasa maeneo ya mijini ambapo chumba kimoja cha bafu kinatumiwa na wanafamilia
wengi,
mabafu ya cubic ndio yanayofaa zaidi. Pia kwa Watanzania wengi ambao hawana
uwezo wa mabafu makubwa au yale yenye sinki la kuogea ukiwa umekaa au umelala,
lakini wanataka kuishi kwenye nyumba za kisasa, mabafu ya cubic yameonekana
kuwa mkombozi mkubwa kwao.
Matumizi mazuri ya maji
Kama
tujuavyo ni vyema kutumia vyema rasilimali ya maji. Kwa ajili mabafu ya cubic
ni ya bomba la mvua matumizi yake ya maji ni kidogo kuliko bafu linguine lolole
liwe ni lile la kubeba ndoo ya maji au la kujaza sinki la kuogea. Kwa bafu la
cubic mtu mzima anaweza kuoga kwa nusu ndoo ya maji tu.
Urahisi wa matumizi
Ili
kutenga eneo maalum la kuogea bafuni, kabla ya mabafu haya wengi waliweka pazia
la bafuni. Endapo utakuwa na bafu la cubic huna haja ya pazia hilo tena.
Yanapendezesha
bafu
Faida nyingine ya bafu za cubic ni kwamba zinakuja
kwa miundo na mitindo mbalimbali. Mabafu
ya cubic yanachukua nafasi ya pambo la bafuni kutokana na kuta zake za vioo vya
kuvutia.
Ni rahisi kusimika
Kusimika
mabafu ya cubic haijalishi mpango wa awali wa chumba cha bafu husika. Hata sasa
endapo una bafu la pazia ni rahisi kulibadilisha na kusimika la cubic. Au kama
una la sinki la kuogea bado kuna kona ambayo unaweza kuongezea la cubic kwani
halichukui nafasi kubwa na eneo la kuingilia na kutokea ni moja tu tena kwa
mlango wa kuteleza.
Yanapatikana kwa
bei tofauti
Yapo mabafu ya cubic yenye matumizi zaidi ya kuogea. Kwa mfano yapo ambayo mfumo wake wa umeme unawezesha kutekenya mwili au kutokwa jasho jingi (sauna). Unaweza kupata bafu la cubic kadri ya matumizi yako kwenye maduka ya vifaa vya bafuni.
Yapo mabafu ya cubic yenye matumizi zaidi ya kuogea. Kwa mfano yapo ambayo mfumo wake wa umeme unawezesha kutekenya mwili au kutokwa jasho jingi (sauna). Unaweza kupata bafu la cubic kadri ya matumizi yako kwenye maduka ya vifaa vya bafuni.
Simu 0755 200023
No comments:
Post a Comment