Kuna
maeneo nyumbani ambayo ni kama sumaku inayovuta vitu vinaavyoingia nyumbani.
Maeneo haya yanakuwa na mrundikano hata ujitahidi kiasi gani kuyafanya yawe
nadhifu. Ila kwakuwa huwezi kuweka kila inchi ya nyumba yako nadhifu kila
sekunde, unaweza kuweka maeneo haya huru na
mrundikano kwa kuyatupia jicho
angalau mara moja kila juma.
1.
Kwenye
jokofu
Kusafisha
jokofu na kulipanga upya kuondoa vyakula vilivyopitwa na muda au kama ni mbogamboga
zilizoharibika na kunyauka inaweza kuwa ni kazi kubwa. Si mbaya kama ukiwa
unatupia jicho kwenye jokofu lako walau mara moja kwa juma ili kuweka mambo
sawa.
2.
Kabati
la nguo
Mara moja kwa juma
hakikisha unaingia kwenye kabati lako la nguo, kunja, tundika na ondoa nguo
ambazo zinazagaazagaa. Pia weka pembeni chochote ambacho unadhani hukihitaji
tena. Hivi unaweza kuvikusanya kwa muda hadi vikiwa vingi ugawe. Hii
inakusaidia kwa ajili kwa juma nzima unajua ni nguo au viatu vipi vinavyokufaa
au visivyokufaa tena.
Kwa wengi wakati wa
kutizama kwenye kabati la nguo wanautumia pia kutembea chumbani kwa ujumla na
kukiweka sawa. Huenda kuna glasi uliyotumia hapo chumbani juma hilo ukasahau kuirudisha mahali pake, ndio muda
sahihi wa kufanya hivyo.
3. Meza ya vipodozi
Kama unatumia kipodozi
cha aina moja kila siku, kuna uwezekano kuwa kuna vingine vingi ambavyo
huvitumii juma hilo. Hakikisha meza yako inabeba vipodozi unavyotumia tu na
kuondoa vile vyote vilivyoisha na pia usivyotumia. Vitu vingine vya kuangalia
kwenye meza hii ni pamoja na vibanio vya nywele, hereni, bangili na mikufu na
hata wakati mwingine dawa zilizopitwa na muda wake au ulishapona kitambo.
Vilevile wakati wa
kupaka vipodozi vipo ambavyo vinamwagika juu ya meza. Wakati huu nao ni mufaka
kwa kusafisha eneo hilo ili kuifanya meza isionekane shaghala baghala.
4.
Stoo
Wengi tunafanya makosa ya kufikiria kuwa stoo inatakiwa kurundikana.
Stoo yoyote iwe ni ya vyakula au vifaa
vya usafi na utunzaji wa nyumba inapaswa kuwa katika mpangilio. Kufanikisha
hili hakikisha kila juma unapitia kwenye stoo zako na kuondoa mrundikano wowote
uliojitengeneza kwa kipindi hicho. Na faida utakayopata ni kwamba utapunguza
kazi kubwa ya baadaye na pia utaepuka uharibifu unaoweza kujitokeza. Kwa mfano
kama stoo ni ya vyakula kama viazi na vitunguu tunajua vyema kwamba vikiwepo
vilivyoharibika bila kuondolewa vinaharibu na vya jirani yake, na vilevile
vinazalisha mende na wadudu ambao wanaendelea kuharibu.
5. Meza ya kahawa
Meza ya kahawa imekuwa
ikionewa kwa kurundikwa vitu kama majarida na magazeti ambayo yamekuwa
yakiwekwa ya leo na kesho yake na kesho kutwa yake. Hali hii inasababisha
mrundikano na kumpa mwenye nyumba au mgeni usumbufu pale anapotaka kuweka
kinywaji chake mezani. Ifanye meza ya kahawa kuepukana na mrundikano kwa
kuitembelea angalao mara moja kila wiki.
6. Droo za jikoni
Ni ukweli kwamba mara
nyingi droo zza jikoni zinachanganyikana vyombo. Eneo lililotakiwa kuwa na
vijiko si ajabu ukakuta kuna kisu kimejichanganya humo. Vilevile droo la
vikontena laweza kuwa limechanganywa sufuria
kwa mfano. Pitia droo za jikoni mara moja kila juma kuhakikisha kuwa
kila chombo kiko mahali pake.
7. Fikra
Unaweza ukashangaa
eneo hili ila ni muhimu kuondoa mrundikano kwenye akili yako pia kadri unavyofanya
kwenye nyumba yako. Ndani ya juma tafakari ni mawazo yapi yanafanya fikra zako
zirundikane na yaondoe kwa kuongeza mengine mapya japo kwa kusoma kitabu! Fikra
za mwenyenyumba zisiporundikana zinamwezesha kuweka nyumba katika mpangilio.
Vivi anakuwezesha kupendezesha nyumba
yako. Simu 0755 200023
No comments:
Post a Comment