Mimea ya kwenye bustani ambayo ni
pamoja na miti, maua na ukoka inahitaji maji kwahivyo majira haya ya mwaka kwa
wapenda bustani ndio wakati sahihi wa kuiboresha. Ni wakati wa vifaa kama chepe,
reki, mkasi, panga, mabuti na toroli kutolewa stoo kwenda kushughuli
kia
bustani. Ni wakati wa kwenda kwenye bustani na kuanza kupunguza miti, maua na
hata kukata majani. Ni wakati wa kuipendezesha bustani katika maeneo mbalimbali
yanayohusiana na upatikanaji maji kwa wingi kwa kipindi chote hiki cha mvua. Na
hata kwa wale waliopanga kuanzisha bustani huu ndio wakati muafaka.
Kipindi hiki ndio kinafaa kwa shughuli
mbalimbali za bustani kama vile kuweka mbolea, kundoa mimea na maua makavu
yaliyozeeka na magugu yanayoshambualia ukoka wako. Wakati huu ni mzuri kwani
ardhi ina maji mengi ya mvua kwahivyo udongo ni mlaini kwa kung’oa
visivyohitajika. Endapo unahitaji kuotesha
maua na mimea mipya, sasa ndio wakati wake. Mizizi itashika kwa kasi
kutokana na mvua zinazonyesha. Ni wakati wa kuziba viraka kwenye maeneo ya
ukoka ambayo yanahitaji kufanyiwa hivyo. Kama kuna mbegu za maua unazotaka
kuanziashia vitalu na vitanda vya maua sasa ndio wakati wake.
Ukiweka
mbolea kwenye ukoka na maua yako kipindi hiki cha mvua ni hakika kuwa utafaidi
matokeo yake kwani maji ya mvua yanarahisisha kuizamisha chini kwenye mizizi.
Kwa
upande wa bustani za kwenye vyungu vya sakafuni ni wakati wa kuotesha upya
mimea jamii ya feni bila kusahau vile vya kuning’inia ambavyo vinahitaji
kuondolewa maua yaliyoharibiwa na kiangazi na kuotesha mapya madogomadogo na
hata waweza kuchanganya kadhaa ya aina tofauti kwenye chungu kimoja mithili ya
kachumbari kwenye sahani, yanapendeza.
Wapo
wenye maeneo ya kukaa kwenye bustani ambapo kuna kivuli lakini mvua ya upepo inaweza
kuharibu viti na mito. Kama ndivyo kwa upande wako, basi yafaa kuviingiza vitu
hivi stoo hadi pale mvua zitakapoisha.
Wakati
huu ni wakati wa kusafisha na kuboresha maeneo mbalimbali ya kisanifu yaliyo
nje ya nyumba yako.
Vivi anakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Simu 0755
200023
No comments:
Post a Comment