Kutokea
sehemu moja au mbili ndani ya jiko, hakuna sehemu inayokusanya harufu kirahisi
kama jokofu. Kuepusha harufu kwenye jokofu sio ngumu kivile ikiwa unajua
unachofanya, kwa kutumia njia sahihi. Endapo jokofu lako litakuwa linatoa
harufu mbaya tumia njia mojawapo kati ya hizi na
hakika tatizo litakwisha.
hakika tatizo litakwisha.
Tafuta chanzo
cha harufu
Wakati
mwingine ni rahisi kusahau ni nini kilichopo kwenye jokofu na kimekuwa huko kwa
muda gani hadi pale unapofungua mlango siku moja na kukutana na harufu ambayo
hujaipenda. Vyakula vinapokaa muda mrefu vina tabia ya kutoa harufu, na
vinaweza kujaza jokofu lako harufu mbaya ajabu. Na hata inapotokea umeondoa
vyakula hivyo, jokofu linaweza kuendelea kutoa harufu kwa wiki kadhaa.
Mara
zote inasemwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba, na ni vivyo hivyo kwa harufu za
kwenye jokofu. Hakikisha vyakula vyote vilivyohifadhiwa ndani yake havijapita
muda wa kutumika. Hii ni kazi ambayo unatakiwa kuifanya angalau kila mara moja
kwa wiki kupitia kwenye jokofu na kuondoa kila ambacho una wasiwasi nacho au
kimepita muda wake.
Hata
kama jokofu litafanyiwa usafi wa uhakika, harufu ndani itaendelea kuwepo hadi
pale utakapoondoa chanzo chake. Chakula chenye hali yoyote isiyo ya kawaida au
kuota kwa ukungu (hasa kwenye mikate) ni wakati wa kuvitupa.
Angalia
shelfu la kuwekea mbogamboga kama kuna matunda yaliyooza au mboga zilizoharibika.
Kama hakukuwa na umeme kwa zaidi ya masaa 24 huenda ukatakiwa kutupa vyakula
kama nyama, samaki na maziwa kwani vinaharibika
ndani ya masaa machache.
Safisha kwa kina
Kama
umeshaondoa vyakula vyote vilivyoharibika na kupita muda wake lakini bado kuna harufu;
ni wakati wa usafi wa kina. Ondoa vyakula vyote kwenye jokofu ili kusafisha
kila mahali kwakuwa huenda vyakula vilivyokuwa vinatoa harufu vilichuruzikia
ndani hadi kwenye kingo za shelfu. Weka vyakula hivyo sehemu ya baridi hata kama
ni kwenye jokofu lingine. Ondoa shelfu zote na zisafishe kwa maji moto na
sabuni. Fanya hivyo pia kwenye kuta, dari na sakafu ya jokofu. Safisha mlango
kwa ndani. Kausha na taulo halafu rudishia mashelfu na hatimaye vyakula.
Harufu
iking’ang’ania
Kama
bado kuna harufu, inaweza kukubidi uondoe vyakula vyote, lizime na kuliacha
mlango wazi kwa siku kadhaa hadi harufu itoweke.
Njia
nyingine zilizothibitika kuweza kuondoa (kuepuka) harufu kwenye jokofu ni kwa
kutumia hamira au mkaa. Fungua pakiti ya hamira uiweke ndani ya jokofu na iache
wazi. Inanyonya harufu zote na kuliacha likiwa na hewa safi. Inakupasa
kubadilisha pakiti ya hamira kila mwezi kwa ajili inaishiwa nguvu ya uendelea
kunyonya baada ya kipindi hicho.
Mkaa
unaondoa harufu kwenye jokofu kwa kudumbukiza kipande ndani ya kikombe chenye
maji halafu unakiweka ndani ya jokofu.
Pia
kuwa kuna deodoranti zinauzwa madukani kwa ajili ya kuweka kwenye majokofu.
Usipochukua
hatua mapema, inawezekana usiweze kuondoa harufu mbaya kwenye jokofu. Ina maana
utakuwa na machaguo mawili ambayo ni ama kuishi na hiyo harufu kwa kuivumilia
au kununua jokofu lingine.
Hata
hivyo baada ya kutumia njia zote hizi kama hamna mafanikio ya harufu kutoweka
na kama jokofu ni mpya na liko kwenye waranti, wasiliana na wauzaji pengine
tatizo ni la kiwandani.
nifollow instagram @vivimachange
No comments:
Post a Comment