Makochi
yanakuja kwenye malighafi mbalimbali za vitambaa pamoja na ngozi ila kwa hapa
tunazungumzia yale makochi ya vitambaa. Vitambaa vingi vya makochi ni vigumu
kusafishika kirahsi bila kuacha alama yoyote ya uchafu. Na wataalam wa
kusafisha wanachaji gharama ambayo pengine huwezi kuimudu. Asante kwa uwepo wa
dawa mbalimbali ambazo unaweza kutumia kusafishia kochi mwenyewe nyumbani.
Kwanza
ili uweze kusafisha kochi la
kitambaa kwa usahihi unapaswa kujua aina ya kitambaa
kilichotengenezea kochi hilo. Kusema kweli makochi mengi ya kutoka nje ya nchi
yana maelezo ya aina ya kitambaa na njia ya kusafisha. Kwa mfano yapo yanayoweza
kusema kuwa safisha na maji , na mengine ni kwa ukavu tuu (dry leaning). Ila
kama umetengenezesha kochi hapa nyumbani inaweza kukupasa kuuliza aina ya
kitambaa na utunzaji wake.
Kwa aina yoyote ile ya usafishaji
hakikisha unaanza kusafisha kochi kwa kuvua zile sehemu zinazovulika ili
uzisafishie pembeni. Kwa mfano kama ni za kusafisha mwenyewe kwa maji na sabuni
au ni kwa ajili ya kusafisha kwa dry cleaner.
Baada ya hapo brashi taka za juu kama vile mchanga, udongo, manyoya ya wanyama
wa kufugwa ndani, na mabaki ya chakula kwa kutumia brashi laini au mashine ya
upepo. Na vilevile sogeza mito ya
kukalia na kusafisha eneo la chini ya mito hiyo kwakuwa taka nyingi
zinadondokea na kujificha humo.
Kama kochi linahusika
na kutumia dawa za kusafishia hakikisha unanunua iliyo sahihi inayosema kuwa
inatumika kusafishia makochi. Zingatia yale maeneo yaliyo chafu zaidi kama vile
panapumzikia kichwa na mikono kwani maeneo haya yanaweza kuhitaji umakini
zaidi.
Kama kitambaa cha kochi kinaruhusu
kutumia maji basi kwa haya maeneo
yaliyobaki ambayo hayavuliki tengeneza povu
na tumia brashi laini, kitambaa au sponji kuendana na kiwango cha uchafu
na kuanza kusugua taratibu. Kumbuka huna haja ya kutumia maji mengi kiasi
kwamba yanachuruzika sakafuni. Baada ya hapo chukua maji matupu bila sabuni na
yakiwa ni ya uvuguvugu yatafaa zaidi, pamoja na taulo jeupe.
Loanisha taulo na anza kufuta kule
ulikosugua na povu hadi taulo linyonye uchafu wote kiasi kwamba mzunguko wa
mwisho hautaoinyesha uchafu wowote kwenye taulo. Uwe makini na kitambaa
kinachochuja ukadhani ni uchafu kumbe sio. Baada ya kujiridhisha kuwa kochi ni
safi kabisa basi ni wakati wa kuliacha likauke aidha kwa kulitoa nje au kwa
kufungua madirisha kuruhusu upepo kuharakisha zoezi hilo.
Tukija kwa kochi lenye maelezo kuwa
lisafishwe kwa dry cleaning tuu, maadam unakuwa umeshaondoa vile vitambaa vya
eneo kubwa ambalo ni lile la kuvulika basi kinachofuata ni kutengeneza
kiniminika cha usafishaji huo na anza kusafisha, baada ya hapo fanya lile zoezi
la kufuta kwa taulo jeupe safi ili kuondoa hicho kimiminika ulichosafishia na
pia kujiridhisha kwamba kochi limetakata kwa kutokuacha uchafu wowote ule
kwenye taulo.
ulizovua kusafishia pembeni vikiwa
tayari valisha upya na hakika unakuwa
na kochi safi.
No comments:
Post a Comment