Naomba ingia instagram @mtotomagazine u like picha hii hapa chini ili ishinde. Asante sana
Maji ni rasilimali muhimu kitaifa na kimataifa. Wazo la kuwa na bustani kavu ni zuri hasa kwa walio maeneo yenye ukame, wasio na maji ya kutosha kumwagilia, na pia wenye pilika nyingi. Hawana muda mwingi wa kutumia katika kutunza bustani, ingawa wanapenda iwe na muonekano mzuri. Kama ndivyo basi suluhisho ni
bustani kavu.
Bustani
kavu ni bustani ambayo sehemu kubwa ya ardhi yake ina mawe badala ya ukoka na
kwa upande wa maua na miti imeoteshwa ile ya kuweza kuhimili ukame. Ni vyema,
kwako wewe unayepanda wazo la bustani kavu kufahamu haya.
Bustani
kavu inakuwa na maua machache ambayo nayo yana uwezo mkubwa wa kustahimili maji
kidogo. Kwahivyo wakati unapotaka kuianziasha, inakupasa kuchagua aina ya maua
na mimea ambayo haihita maji mara kwa mara. Kiasi kwamba unaweza ukayamwagili
angalau mara moja tu kwa wiki au hata baada ya wiki mbili. Unachagua mimea
sahihi inayoweza kukabiliana na tabia nchi. Mabadiliko ya tabia nchi yana uwezekano
mkubwa wa kuleta joto na kiangazi cha
muda mrefu kwa maeneo mengi ya nchi., kwahivyo ni vyema kuwa na mpango
madhubuti wa angalau kuweza kuifanya bustani yako ihimili hali hiyo.
Kuna
mimea na maua mengi ambayo yananawiri kwenye udongo mkavu na kuwa na muonekano
wa kuvutia mno. Mimea na maua haya mingi ni ile yenye majani manene kama jamii
ya kaktasi na aloevera na pia ile yenye majani membamba kama sindano ambayo
yana eneo dogo la kupotezea maji juani. Vilevile ipo yenye majani
yaliyojisokota na hii inasaidia kupunguza ukubwa wa eneo linalochomwa na jua
kwahivyo kuepuka mmea kupoteza maji mengi juani. Wauzaji watakuelekeza kabisa kuwa
mmea, mti au ua hili linashamiri kwenye jua kali na halihitaji maji mengi.
Miti
ambayo kamwe haipotezi kijani chake katika majira yote ya mwaka, kwa mfano miti
inayojulikana kama ya Dodoma ni kiungo muhimu kwenye bustani kavu. Vichaka na
miti ya namna hii inavutia na ni muhimu kuleta upepo tulivu bustanini.
Sehemu
ya ardhi ya bustani kavu inakuwa na mawe badala ya ukoka kama zilivyo bustani
nyingi tulizozoea. Faida ya haya mawe ni kuipa bustani kavu muonekano wa mvuto
na kuepusha vumbi. Unaweza pia kuchagua aina ya mawe asili, kwa mfano meupe au
ya kijivu.
Bustani
kavu ina faida pengine kuliko aina
nyingine zote za bustani, kwa ubunifu wa kutumia mawe, mimea michache, ruhusu
ubunifu wako ufanye kazi ili kurahisisha maisha yako huku ukifurahia kupata
unachokipenda. Bustani kavu iliyooteshwa mimea na maua ya kuchaguliwa kwa umakini
pamoja na mawe yake inawezekana kuwa na muonekano mzuri sana. Na kwa kutengeneza
ya kwako hutakosa amani ya kuingia gharama kubwa ya maji katika majira ambayo
hakuna mvua.
Mawe haya yanapatikana KAYIKAYA HOME FURNITURE & DECOR
Simu 0745 970 044
Mawe haya yanapatikana KAYIKAYA HOME FURNITURE & DECOR
Simu 0745 970 044
No comments:
Post a Comment