Ni rahisi kujisikia uchovu pale unapofikiria
ni vitu gani unavyoweza kuleta ndani ili kuongeza dozi ya rangi kwa njia
rahisi, haraka na gharama nafuu. Rangi inaongeza nguvu na uzuri wa ziada wa
eneo, lakini cha muhimu ni kuamini jicho lako, kujiamini kwenye maamuzi yako,
na usizidishe laa iwe unajaribu uone itakuwaje! Ladha zetu kuhusu rangi
zinahama, zinaongezeka na zinabadilika mara kwa mara. Rangi fulani kwenye
fenicha inaweza kuonekana ni ya kuvutia, lakini je
itakuwaje unatapotaka
kubadilisha rangi za vitu vingine kama vile pazia, kuta na kadhalika huko
mbeleni? Kuongeza dozi ya rangi kwa kutumia vitu na kazi za sanaa ni rahisi na
wigo ni mpana.
Uzuri ni kwamba vitu na kazi za
sanaa zinaweza kuhamishwa kutoka chumba hadi chumba pale unapoamua kwenda na
mtindo mwingine. Usumbufu wa kuhamisha si mkubwa na vilevile bei huwa si za
kutisha ukilinganisha na mfano wa zoezi la kubadilisha rangi ya ukuta, au
kubandua wallpaper ili kubandika nyingine.
Njia ya kwanza ya kuongeza dozi ya
rangi ukutani ni kwa kutumia sanaa, vitu au mapambo madogodogo. Sehemu ikiwa na
mwanga sahihi na unajitahidi kuongeza dozi ya rangi, hebu fikiria picha za ukutani
zenye fremu nyeusi na nyeupe. Changanya picha zako hizo na nyingine mbili au
tatu zenye rangi tofauti, kama unataka rangi za kuwaka fikiria sanaa zenye kazi
nyekundu, chungwa, pinki, njano, bluu na kijani. Na hapo itategemea na ukali wa rangi
unaohitaji. Kumbuka rangi zote hizi nilizotaja zina familia ambapo kuna ukali
wa kiwango tofauti tofauti kuanzia zile nyepesi hadi nzito.
Kuna hii njia
nyingine ya kutumia sanaa chache kubwa endapo kuchagua rangi kwa sanaa ndogondogo
kunakupa shida. Kwa njia hii unaweza ukachagua kitu au sanaa moja au mbili
kubwa za rangi ili kuzitundika kwenye kuta zenye rangi nyepesi. Kuongeza sanaa
moja au mbili zenye rangi nzito kuendana na ukubwa wa ukuta itasaidi
kutengeneza eneo la kitovu kama unafikiria kuhamisha jichoi kutoka kwenye sofa,
fenicha nyingine kubwa au luninga.
Njia ya tatu ni kwa
kuchagua rangi zinazopishana. Hii ni kama kuanzisha mazungumzo kati ya sofa,
meza ya kahama, au maua ya kona na ukuta. Ni kutafuta vitu vya rangi mbalimbali
ndani ya nyumba yako ambavyo vinasaidia kutengeneza mpishano wa rangi katika sehemu
tofauti za chumba na sehemu ya ukuta. Kuchanganya rangi kwa namna hii
kunasaidia kuongeza utajiri wa rangi na hivyo kukamilisha dozi.
Hata kama umebandika wallpaper, bado
unaweza kuongeza vitu va rangi ukutani kwa kuhusisha maua na michoro iliyoko kwenye
wallpaper hiyo.
NIFUATE INSTAGRAM @vivimachange
No comments:
Post a Comment