Mukhangu
Noah ambaye ni fundi milango anasema kuwa kati ya milango inayotengenezwa kwa
malighafi mbalimbali ni muhimu kuchagua milango ya mbao ya mkongo, mninga au
mnazi ukilinganisha na
mingine yote.
Milango
ya mninga na mkongo inaingia kwenye kundi la milango ya mbao ngumu. Tofauti
yake ni kwamba mkongo una madoa doa mengi. Pia ni mgumu mno sio rahisi kupinda
au kutobolewa na mchwa kwa hivyo wenye kujenga nyumba za kisasa wengi
wanapendelea kuutumia mkongo kwenye fremu huku mninga ambao nao ni mbao ngumu
lakini ukiwa wa kuvutia zaidi kimuonekano ndio unaotumika kwenye mlango wenyewe
hasa kwa watu wa bara, wakati wale wa pwani wakibobea kwenye milango ya mbao ya
mnazi.
Mionekano
wa aina hizi tatu za mbao za milango moja kwa moja inapendezesha nyumba kwa
ajili ni mionekano ya asili. Kimsingi namna nyumba yako inavyoonekana
inakusemea wewe ulivyo na ndio maana kila mmoja anatamani kuwa na nyumba yenye
muonekano wa kuvutia kwa kuwa na fenicha, vitupio, mapambo, mpangilio na rangi
nzuri za ukutani za kuvutia. Kwahivyo kitu kama milango pia ikitengenezwa kwa
umakini inaipa nyumba mvuto.
Noah
anasema, ndani ya nyumba milango ya mninga au mnazi inaleta hali nzuri ya
kimuonekano kuliko milango ya aina nyingine yoyote ile. Hizi ni faida kuu za
kuwa na milango ya mbao za mninga:
·
Inatunza
na kuweka hadhi ya nyumba yako katika kiwango kilekile ikiwa mpya hata
itakapozeeka.
·
Inadumu
muda mrefu sana kwani haishambuluwi na wadudu kutokana na ugumu wa mbao yake.
Inaweza kudumu hadi miaka 60.
·
Ni
rahisi kufanyia marekebisho bila mbao ya awali kuharibika.
·
Haina
gharama kubwa ya utunzaji, mkono mpya wa rangi, polishi au mati unatosha bila
kupauka au kuharibiwa.
·
Ina
toa wigo mpana wa urembo wa kuupendezesha kwa mfano kuweka paneli na kadhalika.
Mbao ya mninga haina mwisho wa ubunifu wa urembo.
·
Ni
mgumu, mzito na unahimili msukumo wowote wa nyumba na sio rahisi kupinda. Vivyo
hivyo kwa mnazi, mbao yake ni ngumu sana
na haipindi ikiwa imeshakauka.
·
Inahakikisha
kiwango kikubwa cha usalama dhidi ya mwizi
·
Inaipa
nyumba mguso wa asili
Vivi anakuwezesha
kupendezesha nyumba yako. Piga/whatsapp 0755 200023
No comments:
Post a Comment