Wednesday, March 2, 2016

Mambo matano unayotakiwa kufahamu kabla ya kuanza mradi wa kupendezesha nyumba yako


Hongera! Umeamua kuanza kuipa nyumba yako muonekano wa kuvutia. Kwa binadamu yeyote nyumba ni mali muhimu na ambayo iko karibu zaidi na moyo wake. Kila mwenye nyumba anatamani nyumba yake ionekane nadhifu na ya kuvutia  bila shaka kuliko sehemu yoyote ile nyingine kwenye ulimwengu huu. Hii ndio maana dhana ya kupendezesha nyumba iko kwa kila mtu.

Kama tujuavyo kupendezesha nyumba kunahitaji muda na fedha, hivyo unatakiwa kuwa makini sana na maamuzi yako. Mara tu unapoanza kufikiria jambo hilo, kuna mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya
kuanza mradi wa kupendezesha nyumba yako. Mambo hayo ni haya matano yafuatayo:

1.      Kupanga bajeti
Hili ni jambo muhimu na la kwanza kabisa unalopaswa kuliangalia. Kaa chini na familia yako na mpange bajeti ambayo sio kubwa sana kwako. Kupendezesha nyumba sio kitu kinachotakiwa kufanywa kila mara, kuwa makini na chaguzi zako. Haishauriwi kutumia fungu kubwa la akiba yako kwenye jambo hili. Ingawa bajeti inayotekelezeka inaweza kufanya maajabu ya kupendezesha nyumba yako.

2.      Ainisha mahitaji
Katika swala la kupendezesha nyumba wengi wako makini na wanachotaka. Kila mwenye nyumba ana ladha binafsi anayotaka. Kwa mfano familia zenye watoto wadogo wanapendelea mapambo na fenicha ambazo hazihatarishi maisha ya watoto wao wanapocheza ndani. Wakati huohuo familia zenye watu wazima wakipendea mapambo yasiyo mengi na yenye muonekano wa kiutu uzima zaidi. Kabla hujaanza, aiana mahitaji haya muhimu.

3.      Vifaa maalum
Kutegemea na bajeti yako, huenda una mahitaji maalum katika maeneo maalum ndani ya nyumba yako ili uweze kuifurahia zaidi. Unaweza ukahitaji kuwa na eneo kubwa la luninga na vifaa maalum vya mziki na filamu (home theatre). Orodhesha vifaa maalum na maeneo yake ili kuepuka makosa ya baadaye.

4.      Maeneo maalum
Kutokana na mahitaji binafsi unaweza ukahitaji kuwa na mpango maalum kwenye kila chumba. Muonekano wa chumba cha kulala, jiko, chumba cha chakula na sebule inatofautiana kutokana na matumizi ya kila chumba na umuhimu kilichopewa. Ainisha maeleo maalum na mahitaji yake kabla ya kuanza kuyapendezesha.

5.      Kupata ushauri
Mara nyingi wenye nyumba wengi wanajiuliza kama wanahitaji ushauri au wanaweza kuanza  kufanya wenyewe. Kumbuka kuwa kazi ya kupendezesha nyumba inahitaji uzoefu na kufikiria kwa kina, ambapo vitu hivi viwili muhimu ni mpambaji pekee ndiye anaweza kuwa navyo. Ndiye mwenye uwezo wa kukuonyesha mchoro wa namna mapambo, vifaa, samani , fenicha na uwiano wa rangi utakavyokuwa. Kwahivyo wewe mwenye nyumba unakuwa umeshapata picha ya  muonekano wa chumba kimoja baada ya kingine.


Vivi anakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Simu 0755 200023

No comments:

Post a Comment