Kabati
la nguo kwenze chumba cha kulala ni fenicha muhimu. Ingawa linajulikana kama
kabati la nguo, linahifadhia vitu vingi mbali na nguo. Vitu hivyo ni pamoja na
nguo zenyewe, viatu, masanduku, mabegi, vitupio vya urembo na vitu vingine
vingi ndani za chumba chako hicho hivyo kukuwezesha kuwa na mpangilio wa vitu
chumbani.
Kuna
miundo miwili mikuu ya milango ya makabati ya nguo ambayo kutokana nayo unaweza
kuongeza au kupunguza maeneo ya kuhifadhia. Makabati ya nguo yenye milango ya
kufungua kwa kutelezesha ni mazuri pale ambapo chumba ni kidogo na hakuna eneo
kubwa kuruhusu milango ya kufunguka kwa nje.
Wewe mwenye chumba cha hivi utafurahia zaidi kabati lenye milango ya
muundo huu kwani utabakiwa na eneo kubwa chumbani. Kwa muundo wa pili wa makabati
yenye milango ya kufunguka kwa nje yanakupa wigo mpana zaidi wa eneo la
kuhifadhia ndani ya kabati hilo. Cha msingi kwa aina hii ya kabati ni chumba
kuwa na nafasi ya kutosha kuruhusu milango kufunguka kwa nje na bado wewe au
mwingine akaweza kupita na kupishana vizuri
kwa uhuru chumbani.
Kimsingi
pangilia ndani ya kabati lako la nguo kama ifuatavyo:
·
Kwakuwa ndani ya kabati kuna
vyumba/maeneo mbalimbali kama vile mashelfu ya juu na chini, madroo, fimbo ya
kutundikia nguo na kulabu za kuning’iniza vitu. Kwenye shelfu za chini
utahifadhia viatu endapo hujatundika mfuko wa viatu mlangoni mwa kabati hala
pale milango ya kabati inapokuwa ni ile ya kufungua kwa kutelezesha. Tumia
mashelfu ya juu kuhifadhia masanduku, mabegi na vile vitu ambavyo havitumiki
mara kwa mara.
·
Jitahidi kutumia henga zinazofanana
kwenye nguo zote ulizotundika. Lengo kuu ni matumizi sahihi ya nafasi na kufanya
mpangilio uvutie.
·
Kama hazipo, weka kulabu (hooks)
kwenye milango ya kabati kwa ajili ya kutundika mikanda, kofia, tai, skafu na
mikoba. Hii ni kwa yale makabati yenye milango ya kufunguka kwa nje.
·
Panga nguo ndani ya kabati kwa
makundi: Kundi la blauzi, jaketi, sweta, makoti,shati, suruali, suti, sketi,
gauni, kaptula, fulana na kadhalika.
·
Tumia droo ndogo kuhifadhia soksi na
nguo za ndani.
Kwa mpangilio huu hakika
utalifurahia kabati lako la nguo kwani licha ya kuvutia ni kwamba
litakurahisishia kupata kwa haraka na wepesi kile unachohitaji ndani ya kabati.
Vivi
anakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Simu 0755200023
No comments:
Post a Comment