Ubunifu
ni sanaa, na namna ambavyo unapendezesha mahali unapoishi ndio mfano hai wa
jambo hili. Wakati unapoamua kupendezesha ukuta wa nyumba yako unaweza kuchagua
kati ya rangi na karatasi za ukutani zijulikanazo zaidi kama wallpaper. Vitu
vingi kama rangi, mguso, michoro na maua unaviangalia wakati huo. Ila ukiamua
kuweka wallpaper unapata vitu hivi vyote kwenye kifurushi kimoja.
Kubandika
wallpaper ndio hata rahisi zaidi ukilinganisha na mchakato mzima wa kupaka
rangi.
Hapa
naorodhesha faidia 4 utakazopata kutokana na kubandika wallpaper kwenye ukuta fulani wa
nyumba yako. Faida hizi ni za msingi na si za kudharau:
·
Zinadumu
muda mrefu - Zinafaa kwa matumizi yoyote na kwa mtu yeyote katika chumba chochote
iwe ni bafuni, chumba cha kulala au cha chakula. Wallpaper inaweza kudumu hadi
miaka 15 na hata ukuta ukipata alama ndogo za nyufa, kwenye wallpaper hazitokezi.
·
Rahisi
kusafishika - Ni rahisi mno kusafisha wallpaper kwa kitambaa kilicholoa. Hii
inakusadia kuondoa vumbi au uchafu mwingine kwa haraka mno bila kuacha alama
yoyote ukutani. Na nzuri zaidi unaweza kuchagua aina ya wallpaper ambayo ni
ngumu kiasi kwamba unaweza hata kusafisha kwa sabuni na brashi.
·
Ni
rahisi kubandika na kubandua - Huenda nawe ni mmoja wa wanaohofia kuwa
kubandika au kubandua hizi karatasi za ukutani kutasababusha uharibifu wa
ukuta. Sii kweli, nyingi ni rahisi tu kubandua na kubandika tena kama umeamua
kubadili muonekano kwa kubandua za zamani na kubandika mpya.
·
Gharama
nafuu - Endapo utaamua kubandika wallpaper ni kwamba baada ya muda utagundua
kwamba ingekuwa ni kupaka rangi ungetumia gharama kubwa zaidi. Hii ni kwasababu
wallpaper zinadumu miaka mingi ukutani kinyume na rangi. Pia kama unataka dunia
zote mbili yaani ya wallpaper na ya rangi basi kuta fulani za chumba unabandika
karatasi wakati zile nyingine unapaka rangi.
Uamuzi
wa kuingia kwenye ulimwengu wa wallpaper ni wako wewe mwenye nyumba!
Ninakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Piga/whatsapp 0755
200023
No comments:
Post a Comment