Katika
chumba chochote ndani ya nyumba, pazia linachukua sehemu kubwa ya muonekano kwa
kivyo linaweza kuwa kivutio au likaharibu. Habari njema ni kwamba kuna aina
nyingi za mitindo ya mapazia kuendana na kila nyumba na kila gharama. Yapo
mapazia ya kifahari sana na yapo ya gharama nafuu kabisa.
Ili
kupata matokeo unayoyataka, kuna baadhi ya
mambo ya kuzingatia unapotaka
kununua pazia za chumba cha kulala tofauti na zile za sebuleni au chumba cha
chakula.
Ingawa
wengi wanachukulia kuwa kipaumbele cha kuchagua mapazia ni kuangalia michoro na
rangi kwanza, kiuhalisia hivi ni vitu vya mwisho kabisa kuvitazama wakati
unapotaka kununua pazia kwa ajili ya chumba unacholala. Hii ni kwa sababu,
pazia utakazoweka lazima zina mguso fulani kwenye maisha yako ya hapo chumbani.
Kimsingi
jambo la kwanza kabisa la kuangalia kwa pazia za chumbani ni uzito na unene wa
kutosha kuweza kuzuia mwanga unaoingia
chumbani ukiwa umelala. Mwanga huu unaweza kuwa wa jua la asubuhi ama wa
taa za nje zilizowashwa usiku au hata wa radi. Swala la mwanga linaweza lisiwe
kikwazo kwa wanaoishi vijijini maeneo ambayo nyumba imezungukwa na mimea/miti
mingi, ila ni muhimu sana kwa wanaoishi nyumba zenye uwazi mkubwa nje
unaoruhusu mwanga mwingi kuingia ndani ya nyumba. Pazia kama za pamba na sufi
ni nzito ambazo zinaweza kukidhi vigezo hivi.
Kujaribu
pazia ili kuona linapitisha kiasi gani cha mwanga, ni rahisi kama kuchukua
tochi ndogo ya mfukoni na kumulika kitambaa cha pazia unalotaka kununua. Kwa
jinsi hiyo unatapa uelewa wa kiasi cha mwanga ambacho pazia hiyo inaruhusu.
Ni
muhimu kufahamu pia kuwa pazia zenye rangi za giza au kwa maneno mengine rangi
nzito kama zile za zambarau, bluu na rangi ya udongo zinazuia mwanga zaidi
kuliko zile za rangi nyepesi. Kwa maana hiyo hizi za rangi nzito zinakufaa
zaidi kwenye chumba cha kulala.
Kama
ukiona pazia lenye michoro ambayo hakika umeipenda lakini linaruhusu mwanga
mwingi, ambacho unaweza kufanya ni kulinunua lakini ukaenda kwa fundi cherehani
akaliongezea kitambaa cha rangi nzito kwa ndani. Kitambaa hiki tunakiita lining.
Kwa mfano ukiwa na pazia lenye michoro hiyo unayopenda na ukaweka lining nyeusi
bila shaka utakuwa umenunua pazia unalolipenda na hapohapo likakidhi hitaji la
kuzuia mwanga. Kwa mwingine lining inaweza kuwa gharama mara mbili kwa ajili ukubwa
wake ni sawa na ule wa pazia. Endapo ni hivyo unachoweza kufanya ni kununua
pazia yako uliyopenda japo haikidhi kiwango cha mwanga lakini ukatengeneza
vitambaa vya kufunika madirishani ukiwa umelala. Vitambaa hivi vitakuwa tu sawa
na ukubwa wa dirisha na sio ukubwa wa pazia tofauti na vile vya lining. Wakati
ukiwa umeamka unaondoa vitambaa hivyo na kubakia na pazia lako unalolipenda.
Natumai
umejifunza kitu kutokana na mambo ya kuzingatia kwa ajili ya pazia za chumba
cha kulala. Tukutane makala ijayo.
Vivi
anakkuwezesha kupendezesha nyumba yako. Simu 0755
200023
No comments:
Post a Comment