Huenda
ndio umetoka fungate na umepokea picha zako za harusi, kwahivyo wewe na mume
wako mnaanza kufikiria na kuchambua ambazo mngependa kukuza na kutundika
ukutani. Au labda umepata mtoto na ni wakati wa kumuongeza kwenye hazina ya
picha za familia ulizotundika ukutani. Vyovyote vile, kufremu picha ni sanaa
inayohitaji msanii anayeijua vizuri kazi hiyo.
Fremu
za picha iwe ni za mbao, plastiki au chuma huwa zinahusisha miundo ambayo picha
inapowekwa ndani yake inaruhusu kuwa kivutio kwa wale wanaoitazama. Fremu yenyewe
tu ni sanaa ambapo utakapochagua ya rangi na muundo sahihi bila shaka
inajisimamia yenyewe kabla hata haijawa na picha ya ndani!
Ingawa
ni ukweli kwamba wapo watu wanaonunua fremu na kuweka picha peke yao, ni vyema
kufahamu kuwa msanii wa picha na fremu ana uzoefu na utaalam wa kujua ni fremu
ipi inafaa kwa picha ipi. Na pia anajua hatua sahihi za kupitia ili kufremu
picha katika ubora unaokubalika. Fikiria thamani ya picha zako kwa
maana ya
muda, maandalizi na gharama uliyotumia kuzipiga. Bila shaka usingependa kuwa na
matokeo ya mwisho ambayo hutayafurahia.
Zifuatazo
ni faida za kumhusisha msanii kufremu picha zako badala ya wewe kufanya
mwenyewe:
Kuokoa muda
Unapoamua
kukaa chini na kufremu picha zako, hakuna shaka kuwa utachukua muda mrefu sana
kwani huna uzoefu wa kazi hiyo. Msanii atafanya kwa muda mchache zaidi kwa
kufuata hatua sahihi na mwisho kupata matokeo mazuri kimuonekano na imara kwa
kutokuwa na wasiwasi kwamba labda fremu yako itasambaratika baada ya muda au pengine
ianguke na kuvunjika.
Usahihi wa
kufremu
Hata
kama utanunua fremu zenye mvuto kiasi gani kufremu picha zako mwenyewe ni ngumu
kupatia hasa kwenye kona. Na mtazamaji ataona tofauti tu kati ya picha
uliyofremu wewe na aliyofremu msanii. Hii ni kwasababu msanii ni kazi yake na
anafuata hatua sahihi. Pia ukubwa na muundo wa fremu unahusika kwenye sanaa ya
utundikaji wa picha hizo mara baada ya kuzifremu. Kwa mfano fremu zinazofanana
na kulingana zinapendeza zikiwa eneo moja na katika mstari mmoja. Msanii wa
fremu anajua haya yote ambapo wakati wa kufremu anazingatia matokeo ya mbeleni
pia.
Vilevile
msanii anajua namna ya kufanya picha ya ndani isichezecheze kwenye fremu yake.
Na ni jinsi gani aifunge fremu eneo la nyuma endapo mbeleni utataka kufungua na
kubadili picha. Msanii anajua kioo kipi kitafaa kwa fremu ipi.
Aina za kufremu
Msanii
wa picha na fremu anajua aina mbalimbali za kufremu kutokana na jinsi picha
ilivyo. Zipo picha zenye kingo na zipo ambazo zimejaa kwenye karatasi nzima
yaani hazina kingo, na vilevile msanii mtaalam anajua picha ya ukubwa upi
inaendana na fremu ipi. Bila kusahau
kufremu pia kunatokana na wingi wa sura kwenye picha husika. Kwa mfano endapo
picha ina watu wengi basi fremu inatakiwa kutokuwa na madoido. Vile vile rangi
ya picha inahusika kwamfano kama picha ni ya nyeusi na nyeupe inapendeza kwenye
fremu ya rangi nyeusi na isiyo na madoido. Fremu na aina za kufremu vilevile
zinazingatiwa kwenye kufremu picha za watoto.
Vivi
anakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Simu 0755
200023
No comments:
Post a Comment