Ni rahisi kutozingatia namna pazia na fimbo zake
zinavyofanya chumba kionekane. Ila pale unatapoziondoa ndipo unagundua umuhimu
wake. Zifuatazo ni dondoo chache za namna ya kuchagua fimbo kwa ajili ya pazia unazotaka
kutundika.
Weka fimbo ambazo zinaendana na mapambo mengine ya chumba
husika. Hapa ni muhimu kuangalia rangi ya fimbo. Usijeukanunua fimbo za rangi
ya dhahabu kwa mfano, isioane na
chochote hapo chumbani na ikawa kama kitu kisicho mahali pake.
Zingatia muonekano wa mwisho uliotumika kupendezesha fimbo hizo. Utagundua kuwa fimbo zenye
muonekano usio wa kung’aa wa mati unatengeneza mandhari tulivu kuliko ule wa
kung’aa wa polishi.
Malighafi iliyotumika kutengenezea fimbo sio muhimu sana
kwani pazia ni zilezile hakuna zenye uzito mkubwa wa kutisha useme kwamba fimbo
za malighafi fulani ni imara zaidi kushikilia pazia lako. Kwa hapa hifadhi pesa
yako huna haja ya kununua fimbo za gharama kubwa, zote kazi yake moja.
Cha muhimu
ni kuzingatia urahisi wa kufunga na kufungua pazia ikiwa imetundikwa kwenye
fimbo hiyo. Kwa mfano kuna baadhi ya fimbo haziko laini kuteleza kirahisi
wakati wa kufungua na kufunga pazia ambapo inakubidi kulazimisha.
Uzuri ni
kwamba wauzaji wengi wa fimbo hizi huwa wanauza na mapazia, usiogope
kujaribisha. Ukiona fimbo haiku laini haikufai kwani hutaweza kufungua pazia
zako hadi mwisho kwa uzuri na pia kulazimisha kila wakati itapelekea fimbo
kung’oka.
Angalia ua au tunaita pia vifuniko vya miisho ya fimbo.
Endapo vina muonekano wa mbao (hata kama sio mbao halisi) vitaendana na fenicha
nyingi ambazo huenda unazo chumbani. Chochote utakachochagua cha muhimu ni kuhakikisha
kinaoana na vitu na mapambo ya chumba kizima.
Fahamu muundo wa fimbo unazohitaji. Je, ni zile zilizoko
kwenye seti kwa ajili ya kutundikia pazia mbili, moja nzito na nyingine nyepesi
kwenye dirisha moja au ni zile fimbo zilizoko moja moja kwa ajili ya pazia moja
nzito tuu? Unapaswa kufahamu hilo.
Furaha yangu ni kukuwezesha
kupendezesha nyumba yako. piga/whatsapp 0755 200023
No comments:
Post a Comment