Faida
za kuwa na bustani nyumbani ni nyingi na mojawapo ni kuleta hewa safi katika
mazingira unayoishi. Kama sayansi inavyotuambia kuwa mimea inatumia hewa chafu
na kuzalisha safi. Ili kuwa na bustani
yenye afya kinachoangaliwa sio ukubwa wa jitihada unazoelekeza kwenye bustani hiyo bali
ni namna na wakati sahihi wa kuelekeza jitihada hizo.
Ng’oa
magugu
Magugu
machache hayakwepeki kwenye bustani yoyote ile, ila usiruhusu yashamiri. Ng’oa magugu yatoke na mizizi yake aidha kwa
kutumia kifaa cha kung’olea au kwa mkono mtupu wakati ardhi ikiwa mbichi na
laini. Kama magugu yamekuwa mengi sana kwenye eneo moja, lima eneo hilo na uyaondoe
yote pamoja na mizizi yake ndipo uoteshe ukoka au kama ni maua upya. Mbadala wa
kulima ni kuyaunguza kwa dawa ya kuua magugu ambapo inazama hadi kwenye mizizi.
Zingatia kuwa dawa hizi za kuua magugu zinawezekana pale tu aina ya magugu
inapokuwa imetambulika, ndipo unaweza kutumia dawa husika kukwepa kuunguza uoto
mwingine unayohitajika kubaki.
Kata
majani wakati muafaka
Bustani
yenye afya haikatwi kwa kulazimisha kama baadhi wanavyoweza kudhani kuwa
unapokatia chini sana ndivyo unavyoepuka kukata mara kwa mara. Majani
unayopaswa kukatwa ni yale mepesi ya juu ambayo ndiyo yameongezeka. Ukanda
mnene wa kati na chini unapaswa kubaki vilevile. Pia ni muhimu kufahamu kwamba
usikate majani kabla hujaondoa magugu. Hii ni kwasababu ukakishakata majani huwezi
kuyatambua tena magugu kirahisi kwani kipindi hiki ukoka wote unaonekana sawa. Kwahivyo itakupasa kusubiri
hadi kipindi kingine. Hii ni mbaya kwakuwa magugu yataendelea kuzaliana na
kudhoofisha ukoka sahihi.
Reki
majani makavu yote
Baada
ya kukata majani kuna makosa yanayofanyika ya kuondoa kwa jujujuu majani
yaliyokatwa bila umakini. Hii inasababisha majani hayo makavu kuzama kwenye
vishina na mizizi ya bustani hasa pale umwagiliaji au mvua inaponyesha. Mrundikano
wa majani makavu kwenye vishina na mizizi ya majani hai unafanya bustani
idhoofike. Hii ni kwasababu majani haya
makavu yanazuia hewa kupenya vizuri kwani mimea yote inaihitaji kwa ajili ya
kujitengenezea chakula na ubaya zaidi ni kwamba pia yanaozesha yale mazima.
Tembelea bustani yako kuona kama kuna maeneo yaliyo na mabaki ya majani makavu.
Yareki au yaondoe kwa namna yoyote ile haya kama ni kufagia kwa chelewa.
Bustani itaonekana vibaya lakini baada ya majuma mawili itarejea kwenye afya
tele.
Jaza
uoto maeneo yaliyodhoofika
Kwa
kawaida kuna maeneo ya kwenye bustani yanayoweza kuwa ukoka haujajaa vizuri.
Ongezea mbegu na yamwagilie kuhakikisha mizizi inakomaa kuwe sawa na kwingine.
Mwagilia
na kulisha ukoka
Upe
ukoka unyevu wa kutosha hasa kipindi cha joto kali na ukame. Kama tujuavvyo mimea
inakuwa usiku ni vyema zaidi kumwagilia nyakati za jioni. Endapo utamwagilia
wakati wa jua kali ni kama unapoteza maji yako bure tu. Ilishe bustani yako kwa
kuweka mbolea angalao mara mbili hadi tatu kwa mwaka. Wakati wa masika ndio
mzuri kwa mbolea ili maji ya mvua yaisaidie izame chini kwenye mizizi. Pia ni
vyema kuzingatia muda na kila hatua. Kwa mfano usiweke mbolea bustani ikiwa
bado ina magugu na pia usiweke mbolea ndipo ukate majani. Badala yake weka
mbolea baada ya kufanya hivi vyote.
No comments:
Post a Comment