Japo
wengi wanapendelea kupamba maua yasiyo hai (artificial) ndani ya nyumba, lakini
pia maua haya yanapendeza nje ya nyumba. Ili yavutie inakupasa uchague yale
ambayo kimuonekano yanakaribiana kabisa na yaliyo hai. Yapo maua yasiyo hai ambayo
hadi mtazamaji ayaguse ndipo anaweza kugundua sio hai.
Unaweza
kupata maua yasiyo hai kwa
namna
mbalimbali kama vile mti kamili, majani tu, ua na majani machache yani kishina
na ua na vilevile ua peke yake. Eneo la
nje unaloweka ua lako linaamua matokeo chanya au hasi.
Mara
zote maua haya yanapendeza yakiwa kwenye vyungu vyenye mvuto na si vile vya kawaida
vya kuweka udongo kama vya kuoteshea maua yenye uhai. Vyungu hivi ni vizuri na
gharama kwani vingi ni vya seramiki. Kwahivyo zingatia kwamba watoto wanaocheza
nje hawatavivunja. Kama ni eneo la kuning’iniza kuna vyungu vyenye muonekano
kama wa kiota cha ndege, hivi vinapendeza badala ya vile vya plastiki vya
kuoteshea maua hai. Vinaweza kupeperushwa kama eneo lina upepo mkali, basi weka
mawe ndani kuongeza uzito ili kuhimili upepo.
Uamuzi
wa chungu unategemea lengo hasa la kuweka ua fulani eneo fulani. Kama eneo ni
karibu sana na mwonaji anakopita, yakupasa uweke chungu kizuri kwani wakati
mwingine chungu pekee kinapendezesha bila hata kuwa na ua. Kwa mfano weka
kwenye pande mbili za mlango wa mbele.
Mahali
pengine pa kuweka maua yasiyo hai nje ya nyumba ni katika eneo la kukaa kwenye
bustani. Ning’iniza vyungu vyenye maua yasiyo hai yanayofanana kabisa na hai
jamii ya mitambaazi.
Unaweza
kuchanganya maua hai na yasiyo hai kwa mfano kutupia maua yasiyo hai kwenye
chungu au kitalu cha maua hai na ikaonekana kama vile yale hai ndio yamechanua
yale yasiyo hai, hasa pale haya yasiyo hai yanapokuwa ni ya rangi za kuonekana
sana kama vile meupe, mekundu au njano. Mchanyiko huu unavutia mno na unamchanganya
mtazamaji asiweze kuelewa ni kwa vipi maua yamechanua vizuri hivyo.
Kwa
wale wasiopenda usumbufu wa kumwagilia na pengine udongo kuchafua ukuta, simika
vyungu vya maua yasiyo hai ukutani. Pia mvuto unapatikana pale unapoyawekea taa
za rangi kwa karibu.
Maua
yasiyo na uhai yana faida nyingi kama vile unafuu wa bei na uwezekano wa
kuyabadili wakati wowote unaotaka. Ni rahisi kuyatunza kwa ajili yanaendana na
kila majira hayana cha masika wala kiangazi. Huyamwagilii wala huweki mbolea au
kupulizia dawa za kuua wadudu.
Yametengenezwa
kwa vitambaa vya hariri na mpira kwahivyo hayapauki.
Yapo
ya aina nyingi, unaweza ukapata yoyote unayotaka iwe ni yaliyo kama mimea mitambaazi,
ya kusimama yenyewe au yaliyo pamoja kama kichaka.
Nifuate instagram @vivimachange
No comments:
Post a Comment