Iwe
unaliita kochi au sofa, rangi ya hiyo fenicha kubwa sebuleni kwako inaweza
kuleta matokeo makubwa kwenye muonekano wa chumba hicho. Kama zilivyo fenicha
nyingine kubwa unazonunua kwa ajili ya nyumbani, sofa lako mpya unategemea
kuishi nalo kwa miaka mingi. Sofa, kitanda na meza ya chakula ni fenicha kubwa
tatu nyumbani ambazo zinachukua hela nyingi kuzinunua.
Huenda
ni
nyumba mpya imeshakamilika na sasa umeanza kuweka vitu, ni muhimu kuchagua
sofa kwanza kwani ni rahisi kupamba
kulizunguka. Baadhi ya wenyenyumba wanapendelea rangi ya sofa kuwa ya jamii
moja na ile ya ukuta ili kuleta umoja wa chumba. Hili ni wazo zuri lakini
inaweza kuwa changamoto pale utakapotaka kubadili rangi ya ukuta. Uamuzi mzuri
ni wa kuachagua rangi ya sofa ambayo itaendana na mapambo mengine
yatakayokuwepo sebuleni.
Kwanza
kabisa jiulize je unataka sofa ya rangi nzito au nyepesi?
Wengi
tunasahau kuzingatia rangi ya sakafu pale tunapochagua rangi ya sofa. Kwa mfano
unapochagua sofa ya rangi nzito jiulize je itaendana na zulia la rangi nzito pia
utakaloweka sakafuni? Kwa sababu kawaida sofa ni kubwa na limejaa, la rangi ya nzito/giza
linaweza kunyonya mwanga na ukashangaa chumba kimekuwa cha giza.
Ujanja wa kufanya unapotaka
kujiridhisha na rangi ya sofa ni kununua kipande cha kitambaa chochote cha bei
rahisi kinachofanana na cha rangi ya sofa unayohisi itapendeza ili ukifanyie
majaribio. Chukua japo kiti ukiweke sebuleni unapotaka kuweka sofa halafu
kifunike kwa kitambaa hicho. Ndipo utaona muonekano wa rangi hiyo utakuwaje.
Kizuri ni gharama, unaweza kujipatia mita chache za vitambaa vitatu tofauti
ndipo ukafanya uamuzi. Hiyo itakupa
picha ya rangi itakavyoonekana hapo sebuleni, kama rangi ya sofa itakuwa
nyepesi sana au nzito sana kwa chumba.
Kama unaweka sofa nyeusi kwenye
sakafu nyeusi, itafanya chumba kisionekane. Endapo utaweka sofa ya rangi nzito,
hakikisha sakafu au zulia lina rangi nyepesi kuzidi ya sofa. Meza ya kahawa yenye
rangi nyepesi au ya kioo ndio itafaa kwa sofa hizo nyeusi. Ili kuzisaodia
zionekane.
Sofa ya rangi nyepesi/mwanga ina
changamoto tofauti. Kubwa zikiwa ni kuonyesha madoa na uchakavu kirahisi. Kabla
ya kuchagua sofa nyeupe au rangi nyingine nyepesi, fahamu namna sebule
itakavyotumika kwa hali halisa na sio ya kufikirika. Kama mkakati wako ni kama
wa baadhi wanaochukulia kuwa sofa ni kitanda cha sebuleni basi rangi za
mwanga/nyepesi hazikufai. Lakini ingawa sofa zako zitatumiwa na watoto, kulalia
na kadhalika lakini bado ungependa za rangi za mwangi basi rangi za malighafi
za kuosheka kwa kufuta tu kirahisi zitakuvaa. Au pia sofa za kuvalisha kava za
kuondoa na kufua nazo zitakuwa sahihi kwako.
Ukishaamua kuwa unataka sofa ya
rangi nzito au nyepesi sasa unakuwa ni wakati wa kufikiria rangi halisi. Baadhi
ya watengenezaji, watumiaji na wauzaji wa sofa nilioongea nao wanasema sofa za
rangi zisizoegemea upande wowote (neutral) ndio chaguo la wengi. Sofa zenye
rangi hizo ni rahisi kupamba chumba na zinaonekana kutokupitwa na wakati hata
baada ya miaka kadhaa.
Sofa za rangi zisizoegemea upande
wowote ni pamoja na rangi za krimu, kijivu na ugoro. Sofa za rangi hizi
zinaweza kuendana na mapambo yoyote na bado zikawa na mvuto wa kisasa.
Usisahau rangi za mito na mitandio
utakayotupia kwenye sofa zako mpya.
Simu 0755 200023
No comments:
Post a Comment