Zulia sio ngumu kulitunza kama baadhi ya watu
wanavyofikiri, ila kama ilivyo kwa kitu kingine chochote linapaswa kutunzwa ili
liweze kudumu na kubaki kwenye ubora wake kwa muda mrefu. Kama ndivyo, hivi ni
vitu vitano ambavyo hupaswi kuvifanya kwenye zulio hilo.
Usilisugue kwa
brashi likiwa kavu
Inapotokea
kitu cha kusababisha doa kimemwagika kwenye zulia kwa bahati mbaya ni ukweli
kuwa unahamaki. Kadri unavyoshughulikia doa mapema ndivyo unavyoepusha kulifanya
lisikomae. Sasa basi, badala ya kuhamaki na kukimbilia brashi maji na sabuni, sugua eneo hilo kwa
kutumia maji na sabuni au dawa ya kuondoa madoa kwenye mazulia kwa sponji au
kitambaa. Zulia limetengenezwa kwa nyuzi zenye manyoya zilizosokotwa pamoja ili
kuliongezea uimara. Kwa kusugua manyoya haya kwa brashi inayasababishia
kufumuka na kutengeneza udhaifu kwenye hili eneo na bila shaka pataonekana
tofauti na kwingine.
Unaweza
kujiuliza je inakuwaje tunapopeleka mazulia kusafishwa kwa maji ya msukumo na
brashi? Ni kwamba pale ni zulia lote linasafishwa na sio kisehemu kimoja tu,
kwahivyo ingawaje mfumuko wa nyuzi unakuwepo lakini kwakuwa ni zulia zima
tofauti haionekani. Na pia kumbuka uoshaji huu wa zulia kwa maji mengi unaweza
kuwa unafanyika mara moja au mbili tu kwa mwaka laa zaidi ya hapo kuwe na
sababu maalum.
Usilisafishe kwa
dawa za madukani ambazo sio maalumu kwa zulia
Kuna
dawa, sabuni na kemikali nyingi za kusafishia vifaa mbalimbali vya nyumbani
kama vile za vyombo, za mbao za vioo, za nguo na za kila kitu (multipurpose) Ni
vyema kusafisha zulia kwa kemikali iliyoandikwa kwamba inahusika na kusafisha
zulia. Ilishawahi kutokea kemikali ya kusafisha vioo kwa kutokujua ikasafishia
zulia na matokeo yake ikatengeneza doa la kudumu kwenye zulia lile.
Usitembee na
viatu juu ya zulia
Mazulia
mengi ya nyumbani yametengenezwa kwa manyoya laini ili kuleta hisia nzuri
kwenye nyayo. Si sawa kutembea juu yake ukiwa umevaa viatu. Kuvua viatu
mlangoni kila mara unapoingia ndani ni moja ya njia rahisi na sahihi ya kufanya
zulia lako lidumu. Zaidi utaepuka kuingiza uchafu na rangi za viatu kuacha
alama kwenye zulia (fikiria soli zinazotoa rangi).
Usiburuze
fenicha
Kuburuza
fenicha juu ya zulia hasa linapokuwa lile la ukuta kwa ukuta, inaweza kuonekana
ni njia rahisi ya kuhamisha fenicha hiyo kutoka eneo moja hadi lingine. Ila pia
ni moja ya njia rahisi kabisa kuweka alama kwenye zulia. Nyanyua kitu juu ya zulia
kabla ya kukihamisha, kama ni kizito omba msaada wa mtu mwingine.
Usitumie mashine
ya upepo kila siku
Kimsingi
mashine ya kusafisha zulia inafanya kazi kwa msukumo mkubwa wa upepo ambapo
pamoja na kunyonya vumbi na taka ndogondogo zilizo kwenye zulia, vilevile
inanyonya nyuzinyuzi dhaifu za zulia. Na ndio maana zulia linalonyonywa kila
siku baada ya muda unakuta linakwaruza nyayo badala ya kunesanesa kwa ajili
nyuzi zote laini zimenyonywa na mashine.
Makala
haya yameandaliwa na Vivi. Simu 0755
200023
No comments:
Post a Comment