Monday, October 17, 2016

Namna ya kusafisha milango ya ndani ya mbao

Milango katika nyumba nyingi mara nyingi haifikiriwi kufanyiwa usafi. Ni ile ya vyumba vya kulala, ya makabati ya nguo, ya mabafu, wa jikoni na wa stoo. Labda ni kwasababu haipati uchafu kwa wingi na kwa muda mfupi kama maeneo mengine ya ndani. Hata hivyo inapaswa kusafishwa kila baada ya kipindi fulani. Ikiwa ni pamoja na eneo lenye kitasa linapaswa kusafishwa na
kutakatishwa kwa dawa ya kuua vijidudu kwani kinashikwa na mikono mingi na kila mkono unatofautiana na mwingine kwa kiwango cha usafi. Zifuatazo ni dondoo za namna ya kusafisha milango ya ndani ya mbao, ambapo tunaugawa mlango kwenye maeneo matatu ambayo ni fremu, mlango wenyewe na kitasa.

Anza na kufuta vumbi la juu maeneo yote matatu ya mlango kabla ya kutumia aina yoyote ya kimiminika cha kusafishia. Kurukia moja kwa moja kusafisha kwa kimiminika kutasababisha kusambaza vumbi kwa kutengeneza tope hivyo kuongeza ukubwa wa kazi. Vile vile kuufuta mlango ili kuondoa vumbi na chembechembe za juu za uchafu kwanza, inasaidia kuepuka kuusababishia mikwaruzo na uharibifu.

Baada ya kufuta vumbi, anza kwa kusafisha kuanzia juu kushuka chini fremu iliyozunguka mlango wote. Tumia kitambaa au sponji lililoloa maji matupu ili kuondoa ngazi ya mwanzo ya udongo. Kama fremu hiyo haitakua chafu kivile, maji matupu yanaweza kuondoa uchafu wote.  Laa endapo inahitaji usafi wa kina, tumia maji ya uvuguvugu na sabuni. Ipo milango ambayo inakaa muda mrefu sana bila kusafishwa kiasi kwamba eneo la bawaba linakuwa limeshaanza kuvujisha vilainishi vyake au hata vilainishi hivyo vimeshakauka na kusababisha mlango kupiga kelele pale unapofunguliwa au kufungwa.  Baada ya kusafisha eneo hili la mlango la fremu, tumia kitambaa safi na laini kuikausha ibaki kavu. Kuendana na hali iliyopo unaweza kuhitajika kupaka upya kilainishi kwenye bawaba.

Umeshamaliza kusafisha fremu, sasa unahamia kwenye mlango wenyewe. Kwa ajili unakuwa umeshafuta vumbi unapitia tena hatua hizihizi kama za kusafisha fremu, huku ukikumbuka kusafisha hadi eneo la ubavuni  linaloshikana na fremu. Ni lile ambalo huwezi kuliona mlango ukiwa umefungwa, ingawa linaweza kubeba uchafu mwingi sana.

Ng’arisha mlango wako kwa kutumia ving’arishi vya fenicha za mbao vinavyouzwa madukani.

Malizia kwa kusafisha eneo la tatu la mlango ambalo ni kitasa, kwa kutumia kitambaa chenye unyevu kiasi huku ukiweka umakini wa malighafi iliyotengenezea kitasa hicho. Kwa mfano kama kitasa ni cha brasi unaweza kununua bidhaa maalum zilizotengenezwa kwa ajili ya kusafishia brasi. Mwisho kausha kitasa na kama una dawa ya kuua vijidudu kipake au kipulizie.


Muhimu unaposafisha mlango wa mbao kuepuka kutumia kemikali ambazo hazijaidhinishwa kwa matumizi ya kwenye mbao kwani unaweza kuharibu finishing ya mlango.

Kwa usafi wa majumbani na ofsini waone Cleanex Group simu namba 0713 064 064

No comments:

Post a Comment