Aidha
unapamba upya au ni bahati kwamba ndio umekamisha ujenzi wa nyumba yako, bila
shaka ni wakati wa kufikiria rangi za vitu ambavyo utahitaji kwenye kila
chumba. Vyumba vikubwa kama vile sebule na chumba cha kulala cha wakuu wa
familia ni
kati ya ambavyo vinatakiwa kuwa na ushirikiano kati ya rangi za
pazia na viti.
Kuchagua
rangi ambazo zitashirikiana kati ya vitu hivi viwili ni muhimu ili kuleta
muonekano wa kuvutia na sio tu shangalabaghala kama upinde wa mvua.
Unapochagua
rangi na michoro ya kitambaa cha pazia ni vyema kushirikisha pia rangi na
machoro iliyopo kwenye viti na sofa unapotaka kuweka pazia hizo.
Kwa
kawaida pazia zinatakiwa kuwa nzito na zisizoangaza, unataka kulala katika
chumba ambacho seti yake ya pazia hairuhusu mwanga chumbani au hata kukuondolea
faragha. Itapendeza kama utachagua ambazo zina ushirika na vitambaa
vilivyotengenezea viti na sofa ambapo vinatakiwa kuwa imara, rahisi kusafishika,
visivyodaka uchafu kirahisi na pia visivyopauka na vinene kuliko vitambaa vya
mavazi.
Njia
zifuatazo zitakuwezesha kutengeneza ushirika kati ya rangi na michoro ya pazia
na viti.
Kutumia kitambaa
kinachofanana
Njia
nyepesi zaidi ya kuleta ushirikiano kati ya pazia na viti ni kwa kutumia
kitambaa kinachofanana kwenye vitu hivi viwili. Hii inakifanya chumba kiwe na
umoja kwa upande wa rangi na michoro, inapendeza sana pale hizo pazia na viti
vikiwa pande tofauti za chumba. Kama rangi ya pazia ni nzito, namna nyingine ni
kutumia kwenye viti au sofa kitambaa
ambacho kina rangi ya familia moja. Kwa mfano pazia za bluu nzito zinaweza
zikashirikishwa na vitambaa vya viti vya bluu nyepesi.
Rangi
zinazoshabihiana
Rangi
za pazia na viti zinaweza kushirikiana kwa kutumia rangi ambazo zinaendana
badala ya zile zinazofanana. Rangi zinazoendana huwa ni tofauti kabisa lakini
zikiwa pamoja zinaleta mvuto kwa mfano bluu na nyeupe, zambarau na njano,
nyekundu na nyeupe na pia majenta na chungwa. Kutumia rangi za seti hizi kwenye
pazia na viti kunakifanya chumba kisionekane kulipuka sana ukilinganisha kile
ambacho rangi za pazia na viti zinafanana. Hapo ndio utaona kila jambo lina
faida na changamoto zake.
Rangi
ya kitu kingine
Pazia na viti inaweza kuwekwa kwa jinsi ambayo
italeta ushirikiano kwa kutumia kitu cha tatu kilichopo hapo chumbani. Kwa
mfano kwa kushirikisha rangi ya fenicha au zulia.
Rangi
isiyoegemea upande wowote
Kushirikisha viti na sofa za rangi kwa pazia za
rangi isiyoegemea upande wowote kama vile, krimu, kijivu au nyeusi ni njia
nyingine ya kuleta ushirika wa rangi chumbani. Hapa pazia zinachukua nafasi ya
kutuliza zile rangi za sofa au viti. Kama rangi ya kuta pia ni isiyoegemea
upande wowote basi sofa na viti vinapewa nafasi ya kuchomoza na kuwa kitovu cha
jicho.
Hakika hizi njia nne zitakuwezesha kutengeneza
ushirika mzuri kati ya rangi za pazia na zile za viti na sofa.
No comments:
Post a Comment