Tuesday, June 2, 2015

Kisiwa cha Zanzibar ni Miongoni mwa Visiwa Vitakavyopotea Duniani Kulingana na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Wataalamu wa kichunguzi  na wanasayansi  wa Mazingira, wameelezea kuwa  visiwa vilivyopo ndani ya bahari ya Hindi  vinatarajiwa kutoweka duniani kutokana na mabadiriko ya tabia nchi inayoikumba dunia kwa sasa ikiwemo upungufu wa kimo cha bahari, ukame na hali ya joto sehemu mbalimbali duniani.

Hayo yameelezwa jijini hapa katika mafunzo juu ya kuripoti habari za mazingira na mabadiriko ya tabia nchi (Climate Change) mafunzo yaliyoanza jana Juni 1, 201a5 ambayo ni maalum  kwa wandishi wa habari wanaoandika katika mitandao ya kijamii blog na tovuti kutoka nchi mbalimbali za Afrika, zikiwemo Tanzania, Rwanda, Madagasca, Kenya  na Ufaransa ambaoyo ni ya wiki mbili ambao pia ni mkutano wa maandalizi kuelekea katika kongamano la mazingira litakalofanyika jiji la Paris, Ufaransa, Julai  na Desemba mwaka huu.

Akielezea hali hiyo, Mchambuzi wa mambo ya mazingira katika ukanda wa bahari na mwandishi mwandamizi wa habari  nchini Kenya, Wanjohi Kabukuru, alibainisha kuwa, visiwa vingi ndani ya  bahari ya Hindi ikiwemo Mombasa, Comoro na Madagasca vimo hatarini kutoweka kabisa duniani kutokana na tabia nchi (Climate Change).

“Utafiti mbalimbali umefanyika na kutokana na mabadiliko ya tabia nchi  Dunia itaingia katika matatizo makubwa.  Hasa kwa  upande wa bahari ardhi iliyo ndani yake kuja kumezwa ikiwemo visiwa vya Zanzibar, Madaga” alieleza Kabukuru ambaye pia ni mchambuzi na mtafiti wa masuala ya mazingira ya ukanda wa bahari anayefanya kazi zake nchini Kenya.

Kwa Tanzania tayari athari mbalimbali zimeanza kujitokeza kutokana na tabia nchi ambapo kwa sasa mmomonyomko wa radhi  umeweza kukumba maeneo zaidi ya 148 ambayo yanaingia maji ya chumvi huku wakulima wakishindwa kuendelea na kilimo cha kawaida.


Mkutano huo ulioanza leo Juni Mosi, umeandaliwa na Media Coperation CFI kutoka nchini Ufaransa ulio na lengo la kutafuta njia mbadala juu ya kuripoti habari za mabadiliko ya tabia nchi kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Ufaransa Kenya  na shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), kwa washiriki wa Tanzania,wanawakilishwa na Andrew Chale mtandao wa modewjiblog na Dotto Kahindi  mwandishi wa habari wa kujitegemea.

No comments:

Post a Comment