Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe amesema kama CCM haitampitisha kuingia tano bora, atampigia
kampeni kwa moyo wa dhati Profesa Mark Mwandosya iwapo ataingia fainali ya
kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea urais.
Membe aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na
wanachama   wa CCM kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya
waliojitokeza kumdhamini.
Alisema unapozungumzia viongozi waadilifu nchini, Profesa
Mwandosya ni namba moja, kwani amekuwa kiongozi mwenye maadili ya uongozi na
mwenye upendo wa dhati kwa wengine.
“Natamka hili kwa moyo wangu wa dhati, jina langu
lisiporudi ndani ya chama, nitampigia kampeni Profesa Mwandosya. Sina tatizo
lolote hata  wakisema  mimi nimuachie  Mwandosya nipo tayari,
kwani ndiyo viongozi  wanaotakiwa kama yeye  kwa sasa kuongoza nchi
yetu,” alisema.
Kauli hiyo ni ya kwanza kutolewa na mmoja wa wagombea
urais kwa tiketi ya CCM. Wagombea wengi wamekuwa wakieleza kuwa wameamua
kuingia kwenye mbio hizo kwa kuwa hawajaona mgombea mwenye sifa zaidi yao.
MWANANCHI
 

 
No comments:
Post a Comment