Stamili Mponzi mkazi wa kijiji cha Ikule wilayani
Kilombero,  mkoani Morogoro anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumchoma
mwanae na kumjeruhi mikono kwa madai ya kuiba ugali.
Mama huyo alimuunguza mwanaye 
 Joseph Chawala,
akimtuhumu Kuiba Ugali, kwa mujibu wa watendaji  mbalimbali wa kata ya
Mng’eta.
Wakizungumzia tukio hilo Jerome Chulu na Jeneth Hetela,
 walisema unyanyasaji huo  ulishuhudiwa na majirani wa mwanamke huyo
baada ya kusikia kelele za watoto ambao walimchukua mtoto huyo kumpeleka of isi
 ya mtendaji wa kata,polisi na baadaye hospitali.
Walibainisha baadaye kuwa polisi  walikwenda
kumkamata mwanamke huyo na mumewe Halidi Kiwenji ambaye  inadaiwa alikuwa
karibu wakati wa tukio hilo ingawa baadaye baba huyo aliachiwa ili akawaangalie
watoto wengine nyumbani.
 Polisi  walithibitisha tukio hilo ambalo
uchuguzi wake unaendelea ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo.Wananchi
mbalimbali waliohojiwa wametaka hatua kuchukuliwà kwa watu wanaoendekeza
vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
NIPASHE
 

 
No comments:
Post a Comment